Kuna haja ya kuliboresha zaidi baraza la mitihani la taifa

Joined
May 29, 2012
Posts
89
Reaction score
38
Watu wanalilalamikia baraza la mitihani la taifa (necta).nami nakubaliana nao na naona ipo haja ya kulimulika baraza hilo. Kumekuwa na malalamiko kwamba usahihishaji wa mitihani si wa kuridhisha na baadhi ya watahiniwa hufelishwa kutokana na tabia hiyo, ulipuaji. Kwanza unapokata rufaa ili papers zako zipitiwe wanachukua pesa bure hawasahihishi upya. Pili nadhani si sahihi ukate rufaa kwa necta ileile iliyokufelisha. Kiwepo chombo maalum cha kushughulikia rufaa hizo. Ukweli kuna madudu necta.wanajf mtakapochangia, natoa mifano halisi ya hali hii.ni madudu tupu
 
TRA kuna madudu ya kutisha. NSSF usiseme. NECTA ni chombo pekee nchini kinachofanya kazi kwa uangalizi mkkubwa sana. Tumulike vyombo kama TRA sio kuandama chombo ambachho wafanyakazi wake wanafanya kazi nzuri kwenye mazingira magumu sana ya kifwdha.
 

NECTA imefanikiwa sana kuziba mianya ya kuvuja mitihani. kilichotokea ni kosa la kiufundi ambalo limesharekebishwa. labda tushushe malaika waliendeshe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…