Kuna haja ya kutofautisha Phd za ukweli na ambazo sio za ukweli katika nchi yetu

HISIA KALI

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
694
Reaction score
108
Katika miaka ya hivi karibuni watu wengi wameongeza Dr( PhD) kabla ya majina yao. Ni kweli kuna watu wamestruggle kupata hizo PhDs kwa kukaa darasani na kufanya tafiti kwa muda mrefu, kuna wengine wamejipatia kupitia vyuo uchwara, na kuna wengine wamepewa za heshima. Hizi za heshima hatujua kama walistahili ua la! Sasa kutokana na kuongozeka kwa watu kutumia Phd kama njia ya kujipatia sifa mbele ya jamii na wakati mwingine kupata sifa ambazo wahastahili ninashauri kuwa na sheria inasimamia utumiaji wa hii sifa.

Phd itumiwe tu na watu ambao wamesoma hizo degree kwenye vyuo vinavyotambuliwa na sheria za nchi. Watu walipowe hizo za heshima wasijitambulishe kama Dr.
 

Mkuu kwa waliopitia shule kidogo wanajua kuwa PhD ya heshima na ile ya kusomea zote anaepewa anaweza tumia initial ya Dr...
kama roho yakuuma kwa baadhi ya watu kupewa basi wewe piga msuli uipate darasani....
 
Hoja yako ni nzuri kwa uhai wa kuilinda taaluma na kuipatia heshima inayostahili ila kama hao watakaotunga hiyo sheria ndo watuhumiwa wakubwa unadhani wataitunga? Na wakiitunga kwa shinikizo wataitekeleza?
 
hili nalo ni neono ndugu yangu, mi naomba tuanze kumvua baba ridhi coz hata yake sijajua ameitoa wapi
 
huu ni ukweli bila kupingwa,ni mpuuzi mmnja anayeweza kuthubutu kusema eti roho ya kuuma,ikuume vp wakati tunataka watu wasipewe rushwa za u-Dr,tunataka watu wakae darasani
 
Hata hao waliozipatia madarasani walitakiwa wawe wanazi-defend Doctrates zao kwa ku-verify research zao practically. Yaani applicability ya hizo research. Coz research ni kwa ajili ya maendeleo.
 
Mbona wanatambulika kwa maneno na matendo yao? Hakuna haja ya sijui sheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…