Kuna haja ya nchi kubadili Sheria za uongozi

Kuna haja ya nchi kubadili Sheria za uongozi

Ukiteuliwa na rais kuwa mbunge wewe ni mbunge wa bunge la Tanzania si mbunge wa rais.
Bila kuwa mbunge hauwezi kuchangia mijadala ya ndani ya bunge japo unaweza ukapewa muda kulihutubia bunge. Kumbuka ndani ya bunge kuna Hansard.
Nilichomaanisha kwani hizi Sheria zilizopo sio kama zilishuka Toka mbinguni Bali zilitungwa hivyo tunaweza jitungia TU Sheria mpya kwamba " rais atamteua mtu yoyote kuwa waziri na automatically ataapishwa na spika kuwa mbunge habari itakuwa imesisha hiyo
Kwani hili la rais kuteua wabunge kumi si lilitungwa tu
 
Kwanza kila mkoa ungekuwa Una mbunge mmoja tu.

Then mawaziri wangepatikana kupitia kufanya usahili na sio kuteuana .

Wabunge 300+ wote wanafanya Kazi gani !! Bungeni .
Yani Kuna vitu vinashangaza sana.
 
Hii Mada ina logic kubwa sana na umri mrefu, iko wazi kuwa haitakiwi na viongozi walioshiba na kuvimbiwa.
Itawaharibia ulaji?? Bila kurekebisha baadhi ya mambo katika nchi hii...hatutaweza kupata maendeleo..hiyo mipango ya dira wanayoipanga sio lolote ikiwa tuna mambo ya ajabu ya mihimili kuingiliana...haki huleta maendeleo, wakumbuke
 
Ukiteuliwa na rais kuwa mbunge wewe ni mbunge wa bunge la Tanzania si mbunge wa rais.
Bila kuwa mbunge hauwezi kuchangia mijadala ya ndani ya bunge japo unaweza ukapewa muda kulihutubia bunge. Kumbuka ndani ya bunge kuna Hansard.
Bunge kazi yake ni kutunga SHERIA na kuishauri serikali na kwa maneno mengine kuibana serikali na kuifuatilia...Sasa wewe mbunge ndie serikali....utabanwaje?? Yani wewe mtu mmoja mihimili miwili na kisheria haipaswi kuingiliana?? Haiingii akilini
 
Hakuna mantiki ya Mbunge kuwa waziri,ifike nyakati Waafrika tubadili fikra zetu.
Katika ukanda wa Africa mashariki tumebaki cc tu hatutaki kubadilika majirani zetu kenya, Uganda, Rwanda rais anachaguwa mawaziri nje ya wabunge, wabunge kazi Yao ni kuwajadili na kuwapitisha .
 
1.Jerry Silaa ni mbunge anatumikia mhimili wa bunge ambao unapaswa kujitegemea.

2.Jerry Silaa ni waziri anatumikia serikali ambayo nayo ni mhimili unaojitegemea

3.Jerry Silaa ni wakili wa mahakama kuu hivyo anatumikia mhimili wa mahakama ambao pia hupaswa kujitegemea.

Wakati nikiwa kijana mdogo kabisa zamani tulisoma somo la siasa katika shule za msingi. Nimeskia siku hizi lilifutwa likaja la uraia..katika somo hilo tulifundishwa Kuna mihimili mitatu ya nchi. Serikali, bunge na mahakama. Tulifundishwa kwamba mihimili hii inapaswa kujitegemea na haiingiliani kabisa.

Katika mada yangu hapo juu nimemchagua Jerry Silaa kama mfano. Naangalia wakati akiwa waziri wa ardhi jinsi alivyokuwa anatumia hizo nafasi hadi mihimili inaingiliana katika shughuli zake za kila siku.
Yani waziri anasimama bungeni kwenye mhimili ambapo yeye ni mbunge wa ukonga, akiwakilisha mhimili mmoja wa serikali akiwa minister, huku analaumu mhimili wa tatu wa mahakama kwamba hautendi haki...hauamui vizuri kesi kama yeye mwanasheria na wakili anavyotaka...Yani ni mchanganyiko maalum.

Kuna haja Sasa ya KUBADILI SHERIA zetu.. sio LAZMA waziri atokane na wabunge...ikiwa mihimili hii haitakiwi kuingiliana..vipi waziri atokee kwenye ubunge..Sasa atajibana vipi???

Je ni mnavyoona mihimili hii inajitegemea??

Wasomi karibuni munisahihishe kama nimekosea..

Ngaiwoye nikiwa likizoni sauzafrika
Lakini kweli kuna shida kwenye Sheria zetu apo uwajibikaji hautakuwepo
 
Bunge kazi yake ni kutunga SHERIA na kuishauri serikali na kwa maneno mengine kuibana serikali na kuifuatilia...Sasa wewe mbunge ndie serikali....utabanwaje?? Yani wewe mtu mmoja mihimili miwili na kisheria haipaswi kuingiliana?? Haiingii akilini
Mbunge si mtumishi wa serikali ndiyo sababu serikali haiwezi kumfukuza kazi(ubunge). Mbunge anatakiwa awasilishe serikalini matakwa ya wananchi wake.
 
Mbunge si mtumishi wa serikali ndiyo sababu serikali haiwezi kumfukuza kazi(ubunge). Mbunge anatakiwa awasilishe serikalini matakwa ya wananchi wake.
Kama ndivyo basi tumtenganishe...mbunge awe mbunge, mwakilishi wa wananchi...serikali iwe ni mwingine
 
Mbunge si mtumishi wa serikali ndiyo sababu serikali haiwezi kumfukuza kazi(ubunge). Mbunge anatakiwa awasilishe serikalini matakwa ya wananchi wake.
Mbunge akishateuliwa kuwa Waziri automatically Wananchi wale waliomtuma Bungeni watakuwa wamepokonywa Mwakilishi wao na ule Mhimili uliojichimbia chini zaidi yaani Serikali.

Aliyekabidhiwa kero za Wananchi kuziwakilisha Bungeni anakwenda kugeuka na kuwa mjibu kero za Wananchi. Hapo kwako unaona ni sawa?? Ndiyo maana tunasema tunahitaji Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom