Kuna haja ya Rais Samia kufundishwa jinsi ya kudhibiti hisia zake anapoongea/anapohutubia

Kuna haja ya Rais Samia kufundishwa jinsi ya kudhibiti hisia zake anapoongea/anapohutubia

Umri wangu hauna mantiki katika hili swala. Kuhusiana na hao uliowataja, walijibu hoja ya msingi hata kama walitumia ukali.
Rejea tena hiyo clip halafu uone kama swali lilijibiwa ndugu. Tujaribu kutofautisha mahaba na ufuasi. Wengi wanaohalalisha ujibuji wa mama ni wale wafuasi ambao lolote likisemwa kinyume na kusifia basi wanachukulia kuwa mpendwa wao kapingwa ama kadharaulika.
Umri wako muhimu sana maana ndiyo unaweza kuonyesha kama swali lilijibiwa au halikujibiwa. Katafute majibu ya Mkapa alipoulizwa kuhusu mauaji ya Pemba 2001. Katafute majibu ya Kikwete katika mdahalo kabla ya uchaguzi aliyoulizwa na Rose Mwakitwange, sikwambii majibu ya JPM kwa Pascal Mayalla ndipo utaelewa hayo majibu yana maana gani. Tena hapo nimekutajia kwa uchache.
 
Chadema mmeishiwa nguvu. Suala la katiba mwachieni rais mwenyewe ataliamua.


CHADEMA ni KIRUSI

Haya tunayopitia, ni heri tu ccm iendelee kutuongoza. Chadema mtatugawa, chama chenyewe cha kaskazini mhhhh!!!!! Hapana aise ni bora CUF au ACT lakini co chadema, tlp wala nccr mageuzi.
Hapana na Ndiyo> Nakataa kwamba Katiba ni maamuzi ya rais. Nchi siyo familia ya Samia na katiba siyo ya rais wa ikulu. ni katiba ya nchi!
Nakubali kwamba Katiba siyo kazi ya CHADEMA ni wote! Hivyo CHADEMA hawawezi kujidai eti ni ajenda yao. Tatizo la ukabila hilo wanalo, tena sana! Waiosoma na ambao hawajasoma. Kubebana hadi mikoa ya wengine hadi makanisani, hadi CHADEMA.
 
Umri wako muhimu sana maana ndiyo unaweza kuonyesha kama swali lilijibiwa au halikujibiwa. Katafute majibu ya Mkapa alipoulizwa kuhusu mauaji ya Pemba 2001. Katafute majibu ya Kikwete katika mdahalo kabla ya uchaguzi aliyoulizwa na Rose Mwakitwange, sikwambii majibu ya JPM kwa Pascal Mayalla ndipo utaelewa hayo majibu yana maana gani. Tena hapo nimekutajia kwa uchache.
Ondoa Mkapa, hao Kikwete na JPM siyo watu wa mfano mzuri. Kikwete na JPM walikuwa ni moja ya marais wa hovyo kupata kutokea.
 
Nimeangalia clip kadhaa Mama akiwa aidha anaongea ama anahojiwa, kuna hali anakuwa nayo anapojibu maswali ya kuonyesha kutoweza kudhibiti hisia zake.

Kama kiongozi anapaswa kuwa na busara ya kujua 'tone' ya sauti yake tu inaweza leta tafsiri tofauti.

Huwa anatoa majibu kama vile ana ugomvi binafsi na anaemuuliza.

Kuna zile kauli kama vile "anasutana na mtu", kitu ambacho hakileti tafsiri nzuri.

Kuwa kwake raisi sio siri tena, wote tunajua hivyo hana sababu ya kutumia kila nafasi kuonyesha kuwa yeye ni raisi, hii inaleta tafsiri moja tu; kuwa hajiamini.

Wale watu wa Political Manners and Etiquettes wanapaswa wamuweke chini na kumfundisha jinsi ya kujiconduct in public.

Inapaswa ajue kuwa kama Raisi, hisia zake binafsi sio hisia za kila mtu.

Afadhari mara 100 ya Samia kuliko yule alietoweka kwenye uso wa Dunia.
Samia Ni mstaraabu sana kulinganisha na yule.
 
Umeona kitu nilichokua nakiona,mihemko kwa maswali asiyopenda.body language.
 
Back
Top Bottom