Kuna haja ya vyombo husika kuchunguza zile kambi za Simba nje ya nchi

Kuna haja ya vyombo husika kuchunguza zile kambi za Simba nje ya nchi

Jidanganye kwanini mabadiliko lazima yapitie Serikalini, yule kocha wa makipa alikua wa timu gani,TFF yenyewe ipo under FIFA ila jiulize kwanini Malinzi alibananishwa
Kwa hio leo hii Serikali inaweza chunguza Azam Fc kwa rushwa ?

Mabadiliko yanapitia serikalin kwa sababu ya sheria ya ushindani (FCC) Au huijui hio ?

TFF ipo chini ya wizara ya michezo, ila Team ni pvt bodies
 
Huu ni ushauri tu kwa vyombo husika vinajifahamu siwezi kuvitaja hapa. Ila kwa kifupi kuna haja ya kuchunguza zile kambi za nje za Simba wanaenda kwa minajili gani, tunaelewa humu kwenye football kuna uovu mwingi sana umejificha kama vile, Kamari, Rushwa, Upangaji wa matokeo na pia biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Ukiangalia mchezo wa Jumapili ambapo Simba ilipokea kichapo cha goli 5 kutoka kwa kubwa la maadui Yanga na jana walipoenda na Namungo droo ya moja moja unaweza kudhani Yanga au Namungo ndio walikua nje ya nchi, kwa simba hakuna kinachoonekana cha kimpira hakuna jipya kabisa sasa kama wanaenda nje kuweka kambi na matokeo yake ni kula goli tano mimi na wewe tujiulize huko nje wanakwenda kufanya nini?

Mimi na wewe sio wageni tumesikia baadhi ya viongozi wa Soka wakikamatwa kwa kujihushisha na biashara haramu za madawa ya kulevya Matajiri wengi sana wanapenda kutumia mpira wa soka kama kichaka chao cha kujificha kwa kufanya biashara chafu kwa kigezo kikinuka mashabiki wa timu husika watakua upande wao.

Simba kama wanakimbilia nje ya nchi kwa kigezo cha kambi then mwisho wa siku wanarudi na kuaibisha taifa wanaenda kufanya nini huko nje si bora wakawa wanaweka kambi bunju na hizo hela watumie kufanya usajili.

Roma ikisema imesema.
Post yako inanuka uvundo wa chuki, wivu na ujinga.

Maisha yamenifunza ukiona mtu anatuhumu sana wengine kwa jambo fulani, mara nyingi yeye ndiye mtuhumiwa namba moja.

Unasema Simba wanakimbilia kuweka kambi nje halafu wanakuja kuliaibisha taifa, wameaibisha taifa kwa lipi? Kufungwa na Yanga katika ligi ya ndani kuna uhusiano gani na hadhi ya taifa?

Sipendagi kutumia maneno haya kwa mtu yeyote ila wewe ni mjinga.
 
Back
Top Bottom