Kuna haja ya wasanii wa bongo kuwa wabunifu kwenye matamasha

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Moja Kati ya Jambo nimeona Kuna improvement kwenye mziki wetu ni suala la ubunifu wa majukwaa na hii imechangiwa na competition ya matamasha yetu especially Wasafi festival na fiesta kwa upande wa efm kidogo wapo nyuma kwenye kutengeneza jukwaa lenye kiwango Cha kimataifa.

Ukiangalia Wasafi festival ya dar jukwaa lilikuwa very amaizing unaona kabisa walijipanga hata ukiangalia show ya miaka 10 ya diamond aliyoifanya kigoma jukwaa lilitengenezwa mfano wa castle fulani yenye ghorofa msanii anaweza kupanda juu na kufanya performance yake hata wale walionyuma sana kumuona vizuri msanii kingine zaidi kilichomvutia wasanii wanatokea ndani ya hiyo castle badala ya kuwa na back stage Kama tulivyozoea kwenye matamasha mengi.

Ukija kwenye tamasha la fiesta kwa Mara ya kwanza fiesta iliyofanyika uwanja wa uhuru jukwaa lilikuwa amaizing kuliko majukwaa waliyowahi kutengeneza miaka iliyopita na hii imekuja kutokana na changamoto walioipata kutoka Wasafi festival.

Kuna eneo moja matamasha yote yanashindwa kuyafanyia kazi ndo mainly topic yangu ni suala la performance za wasanii kuwa mbovu ubunifu zero kwa waliowengi.Unaweza kukuta tamasha linawasanii 16 walioperform vizuri ni 5 tu yaani mambo ya ajabu ajabu tu wanayofanya Mara mshabiki unaambiwa uvue shati upeperushe juu yaani umetoa hela yako mwenyewe alafu aitoshi eti nivue shati.

Ukiachana na hilo Kuna wengine wanalazimisha kufanya live band alafu hawajui sometime unakuta vyombo vya bendi sio vizuri ngoma ya zuku alafu inasikika ya bolingo usikii real music.Pia unakuta msanii aendi sawa na back vocal wake na Kuna wengine wanafanya live band Kama gogo mtu mwenye kustahili kufanya Kama hivyo mtu Kama Adele wa Marekani cos mziki wake unataka hivyo lakini bongo mtu kasimama Kama gogo alafu anaimba wakati mziki wake utaki hivyo.

NB: ifike kipindi wasanii badilikeni ili mshabiki anaeenda kuangalia tamasha aone thamani yake ya hela aliyolipia imetumika vizuri.
 
Binafsi sipendi kuamrishwa amrishwa, huwa nasikitika sana kuona wasanii wanawapelekesha mashabiki. Mara fanya hivi mara vile. Mtu analipa pesa na pesa yake hiyohiyo inamnyanyasa. Hii ni sababukubwa ya mimi kutokuwa mdau wa matamasha ya muziki wa bongo.
 
Tatizo pesa mkuu....drake kila show moja stage tu huwa inagharimu kuanzia usd 500,000 utaweza mlipa vizuri huyo msaniii akupe mambo mazuri
 
Hapo kwa live band kushuka chini boss wako ujumbe umfikie
 

We mnyamwezi na wajina mwenzangu badilika mkuu
 
Kulia kushoto mara huku mashariki magharibi....sema woyoooo woyooooo piga keleleeeeeeeeeeeee tunaimba si ndiooooooo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee baba umenichekesha nimecheka mpaka watu wananishangaa aisee eti piga keleleeeeee tunaimba si ndiooo naona umewashika wasanii kunako kiukwel waboa ile mbaya.
 
Kiba sijawah ona show yake
Kiba nae nimemgusa kwenye uzi wangu ukiwa makini na mfuatiliaji wa show za wasanii utajua. kiufupi wasanii hawapo kwenye huo upuuzi ni Ruby, Rama Dee na jide.
 
'jukwaa lilitengenezwa mfano wa castle fulani yenye ghorofa'

Hapana,Jukwaa lilitengenezwa kama msikiti vile.

dodge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…