Kuna hatari naanza kuiona: Kuwa na viongozi waandamizi waliotumbuliwa wengi huku mitaani. Serikali iwe macho nao!

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,153
Reaction score
3,800
Tumbua, teua,tumbua ni dhana njema ya kupanga safu bora ya viongozi.

Hawa wanaotumbuliwa wengi wao hawakupenda itokee na wanatoka kwa shingo upande.

Kuna RC mmoja wa mkoa mmoja alimlilia mtumbuaji, tena alikuwa Dr. kuwa mimi sijui kazi nyingine ya kufanya, ungenihurumia! Kilio hakikusikika.

Kuna wengine wametumbuliwa wakiwa na nafasi nyeti kitaifa tunao mitaani wanajimwaga hadi tunajua na X Y Z za nchi.

Hawa niikumbushe Serikali yangu, siyo wema kwa kukaa vijiweni. Aidha kuwe na uchaguzi makini wa nani akae wapi ili kuwe na tija na kupunguza tumbua tumbua.
 
Wanajua vzr nini maana ya kula kiapo cha kutunza SIRI za serikali na wanaelewa vzr zaidi consequences za kwenda kinyume na kiapo chao.

So wao waje mtaani wapambane maana walishapiga mpunga mnene huko Serikalini na tusisahau tembo hata akikondaje hawezi kua kama sisimizi.

Kama hawakupiga mpunga vzr then kuna vitambulisho vya Magufuli vitawasaidia kupambana na mtaa.

dodge
 
Hapo kwenye vitambulisho umenichekesha.
 
Asikudanganye mtu watumishi wengi hawawezi ishi nje ya kuajiriwa
 

Kikwete aliteua baraza la mawaziri karibu wabunge wote wa CCM, mpaka anatoka 2010 ni wabunge wachache sana walikuwa hawajaukwaa uwaziri.
 
Uko sahihi! Kuvujisha taarifa nyeti za taifa lako ni usaliti unaoadhibiwa vikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…