Wananchi na wanachama wa CCM msipokuwa makini ,kuna hatari ya chama kutoka kuwa chama cha mapinduzi na kuwa chama cha familia na koo tu.
Hapa nazungumzia hasa katika ngazi ya juu ya kiutawala ya chama hiki, nafasi ya Urais katika utawala na siasa.
Familia fulani na koo fulani zinaelekea kukikumbata chama.
Najua hamuwezi kunielewa kwa sasa, ila baadae mtaelewa.
Tayari ipo kama genge la Mafia. Sababu kupitia CCM, Tanzania ipo kwa ajili ya familia chache, kadhaa ikiongozwa na Don, underboss,capos, soldiers, associates chini kabisa wapo machawa wanatoa sifa na kudaka makombo, favour za hapana pale.
Mfumo huu upo kwa ajili ya watu wachache kule juu na familia zao, washikaji, ndugu, marafiki. Wengine wote huku chini wanafanya kazi, biashara kukusanya na kulipa kodi kwa ajili na kwa niaba ya familia chache zilizopo juu.
Mafia ni mfumo wa kibabe, usio wa kidemokrasia. Hautegemea wala kuamini katika demokrasia, uhuru, haki au uwazi kupata viongozi wa ndani na taifa. Bali unategemea maneno ya mtu mmoja mungu-mtu, Don, nguvu, vitisho, utekaji, utesaji mauaji, wizi, ujambazi, rushwa, visasi, magereza ili kuendeleza utawala wao. Ingawa hadharani wanahubiri, haki, demokrasia, uhuru, uwazi kiutendaji hawaamini katika ukweli na haki.
Vigezo wanavyotumia kuchagua viongozi ni kama vinavyotumika kwenye genge lolote la Mafia.