Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Hapa kuna wadau wametoa hpja mbili na mimi nijikite humohumo

A. Mmoja kasema tatizo siyo busara wala nini tatizo ni madaktari. Hilo naafikiana nalo kuwa ni madaktari au wahusika wowote wa mambo hayo mfano viongozi wa dini, kijamii na kimila.

Kulitakiwa kujengwe hali/mazingira ya kukubaliana na kifo kwamba mtu akitokea kuonekana na dalili zote basi tufikie ukomo wa kumhangaikia na siyo kumhangaikia mpaka kujiumiza nyinyi wazima msioumwa

Ukitaka kujua sisi hatujajengwa vizuri kwenye maswala hayo angalia 'Wengine' wakifiwa; wanalia kistaarabu tu ile kupunguza machungu ila M'bongo akifiwa sasa; utasikia uuuuuuwii! Hotateeeee weeeee hoootraaataraatraaaaa homameeeee weee! Yaani atataja mizimu yote na kama haitoshi atararua nguo zake bado chini atajigaragaza na mapepo atapandisha hapo bado kamasi plus homa plus...

Au angalia mfano M'bongo akiwa anaumwa halafu cheki hao wanaokuja kumcheki/ kumjulia hali sasa; badala ya kumfariji na kumpa huduma fulanifulani mgonjwa wao ni kujisuwaniza na kujisunja tu yaani mpaka tena mgonjwa ndo anawaonea huruma wao eti! (Samahani nimechanganyia na kiluga)

Hiyo inasababisha watu wanapukutika kiuchumi sana katika kumnusuru mgonjwa na maradhi fulani na hata mtu akifa bado inaonekana ameonewa sana kufa (regardless miaka 70 aliyonayo) hivyo bado wataendelea kupoteza mali kwa 'wataalamu' kutafuta aliye nyuma ya kifo hicho (mchawi) ni nani

Hoja hapo ni watu (hasa madokta) waseme tu ukweli kama mgonjwa amegundulika kuwa na homa ambayo ni 50 kwa 50 uhai na si kuwa-uplift watu halafu baadae ionekane kufa ni uonevu

B. Jambo la pili kuna mdau amesapoti na kusema eti ni sahihi tu kuuza/ kupukutisha mali zote ilimradi kumtibu au kuhangaikia mgonjwa, tena hakuishia hapo akasema tusiige uzungu bali tujikite kwenye Uafrika wetu kwamba hawa wanaobaki basi kuna wajomba, maanti, mababu, na kadhalika eti watawahudumia!!! Shame!

Mjomba kama unaishi kwa kutegemea hivyo kwanza pole sana halafu pili jiandae kuja kutemewa mate na wategemezi wako hapohapo kwenye kaburi utakalozikwa

Ni kweli kuna mtu kum'beba ndugu yake au ndugu wa babu baba na hata ndugu wa mama yake lakini siyo kihivyo aisee! Utawaachia watu jAnga
 
Mleta mada nilikusihi kwamba unaumwa akili... lakini nataka niseme kwamba sikumaanisha nikuudhi... nilitaka niku engage ili tujadili zaidi kwa nini nimesema hivyo... hata hivyo, kuambiwa unaumwa akili sio tusi...Nimesha futa hiyo post yangu na utanisamehe hata kama hatujuani kwani kama ulisikia uchungu hata kidogo, ninaamini kwamba uwajibikaji baada ya kufa itanihusu...lakini ndio binadamu tulivyo, tunatenda makosa kila wakati... nisamehe bure..

Wazo lako kwenye hii mada ni haki yako na waliotofautiana na wewe nae wana haki yao... mara zingine, wote wanakuwa sawa tu, ila mmoja anakuwa sawa zaidi kutokana na hali halisi ya ile issue husika...

Have a blessed Sunday...



Sent using Jamii Forums mobile app
 
How can you compare life and money wakati Mali zenyewe tunaziacha.
Unaziacha wewe unayekufa!

Kumbuka kuna watoto wadogo wasio na pa kwenda! Unauza nyumba halafu??

Busara inapaswa kutumika hapa na kujua lipi ni bora zaidi!

Uchague kati ya mzee wa miaka 70 na mayatima wadogo wasiojua kesho watalala wapi!

Mambo ya kucheza biko hapana!
 
Sawa mkuu. Yameisha. Uwe na siku njema pia. One love.
 
Kuna kipindi ni muhimu kukubali kwamba kifo kwa ujuzi wetu wa sasa hakiepukiki, na kuna watu wataendelea kuishi baada ya mtu kufariki, hivyo, inaweza kuwa busara kuweka mbele interests za watakaobaki.

Hususan kama mgonjwa anaumwa ugonjwa chronic na kashakuwa mtu mzima.

Mimi siwezi kubariki wazo la kuuza nyumba zangu nilizohangaikia maisha yangu yote, zije kuwa nguzo ya kusaidia uchumi wa kizazi changu na ndugu zangu wa karibu, ili tu niongeze miaka michache katika maisha yangu.

Kitu cha muhimu kabisa ni kujiweka katika mazingira ambayo hatuhitaji kuchagua kimoja kati ya mawili haya, na tunaweza kufanya yote. Kujihudumia matibabu bila kufikia hatua ya kufanya kitu kama kuuza nyumba.
 
Umenena vema sana mkuu...
 
Kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike
Hii Mada yako iko sawa; Labda ila nadhani inategemeana na Potential ya Mtu; Mfano mtu alikuwa ni mpambanaji (potential) hili lazima liangaliwe kwanza kupambana kuhakikisha anatoboa,
Sasa unakuta watu wanapambana na Mtu wa 90, of which kama Busara alishawaachia wenye umri mdogo, lakini hela inatumika nyingi sana tena kwa kuchangishana binafsi sionagi umuhimu wake.

Kama Hela ya Matibabu ya muda mrefu ipo na si tatizo miongoni mwa wanafamilia, then atibiwe tu mpaka umauti utakapomfiika.
 
Hakunaga umuhimu kabisa kwa watu wanaotoka katika familia ya kipato duni/cha chini...
 
Ninaomba kutilia mkazo tu kwamba, watoto wadogo ni lazima wapewe kipaumbele kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…