Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Na hata sisi tukiumwa tuache kuwa wabinafs umesha enjoy life san mpk 65 afu unaumwa na possibility ya kupona ni ndogo au hata ukipona utairudisha familia nyuma sana

Mgonjwa inabidi uwe na huruma na unaowaacha waambie tu ukwel mimi nitangulizen mbele ya haki kwa namn yeyote ile

Kuumwa ni ibada na ikitokea tumeumwa kwa kiasi hicho bas tujaribu kuwafikiria na tunaowaacha watakuwa katika hali gan pind tukiwaacha
 
Kwani kaburini tunaenda na mali? Pigania uhai hata kama utabakiwa na sifuri. Kuna watoto kibao wanazaliwa wazazi hawana nyumba na MUNGU huwatafutia njia.
Hii ya kusema kwamba Mungu atawapa tena licha ya kutoka kuwa na nyumba kisha kurudi kupanga chumba na sebule inahitaji mtu mwenye imani kubwa sana kama wale wazee wa kwenye biblia.
 
Kwa sisi tunao amini Dini na ndiyo usawa huu, ni kosa kubwa sana kukata tamaa katika neema za Mola muumba. Sababu yeye ni muweza wa yote.

Cha msingi ni kupambana mpaka nukta ya mwisho.

Mali hutafutwa kama hawakuwa nazo hapo mwanzo kisha wakawa nazo, kisha wakapoteza mali hizo, hilo si jambo baya tena uzuri zimetumika katika jitihada ya kuokoa maisha ya mtu wao, haina shida. Kwahiyo waendelee kupambana na wasikate tamaa, watapata tena na mambo yatakuwa sawa.
 
Kwa sisi tunao amini Dini na ndiyo usawa huu, ni kosa kubwa sana kukata tamaa katika neema za Mola muumba. Sababu yeye ni muweza wa yote.

Cha msingi ni kupambana mpaka nukta ya mwisho.
Sawa mkuu...
 
Hii ya kusema kwamba Mungu atawapa tena licha ya kutoka kuwa na nyumba kisha kurudi kupanga chumba na sebule inahitaji mtu mwenye imani kubwa sana kama wale wazee wa kwenye biblia.
Mbona una imani kuwa ukimwacha mgonjwa afe ili nyumba ibaki aliyeachiwa nyumba hatakufa karibuni ila yeye na familia wataishi maisha bila kuhangaika na kodi? Kwani ni ww unayetoa pumzi?
 
Asante kwa busara zako mkuu
 
Mbona una imani kuwa ukimwacha mgonjwa afe ili nyumba ibaki aliyeachiwa nyumba hatakufa karibuni ila yeye na familia wataishi maisha bila kuhangaika na kodi? Kwani ni ww unayetoa pumzi?
Mkuu, sipingani na hoja yako kwa maana ina mashiko na mantiki sana ndio maana nikasema inategemeana na imani ya mhusika/wahusika.
 
Hii ndio busara yenyewe mkuu...
 
SOJA hapa nmekuvua vyeo...mwambie huyo jamaa yako asikae vijiweni apambane..kwa umri wake ilibidi awe amewatafutia maisha wazazi wake badala ya kuwaza nyumba kuuzwa..ideally ilijengwa na mzee mwenyewe... pesa ni mapito tu...Unataka nambia mzee upo tayari hata kuua mzazi wako au mtoto kusudi uwe kama ginimbi..maana kama unaweza acha mzazi,mtoto afe kuokoa mali huna tofauti na anayeenda kwa mganga kutafuta fedha za majini
 
Kifo kiko so overated mpaka inakera.
nisimple sana kua kila mtu atakufa nakama unabahati wataanza bibi na babu zako watafata wazazi wako utafata wewe nabaadae watafata watoto wako.

Namuunga mkono soja mdogo nivzur busara ziwe zinatumika
 
Watoto wadogo wakiachwa bila pahala pa kuishi ni mzigo mzito sana kwa familia
 
Kuna vitu vingine kwa sisi waafrika hufanyika kutokana na ujinga wetu. Sasa doctor kakwambia utakufa, mnalazimisha nini? Istoshe asilimia kubwa ndiyo uhamia kwa waganga wa kienyeji na wazee wa upako
Doctor sio Mungu
 
Kuna vitu vingine kwa sisi waafrika hufanyika kutokana na ujinga wetu. Sasa doctor kakwambia utakufa, mnalazimisha nini? Istoshe asilimia kubwa ndiyo uhamia kwa waganga wa kienyeji na wazee wa upako
Kazi ya doctor si kutamka mgonjwa atakufa ni kutibu

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon alikaa ICU akiwa kwenye machine ya kupumlia hewa hajitambui kwa miaka nane bila kujitambua kuanzia 2006 hadi 2014 alipofariki akiwa huko huko ICU
 
Watoto wadogo wakiachwa bila pahala pa kuishi ni mzigo mzito sana kwa familia
Familia za kibwege ndio huwa mzigo ila familia wanaojaliana wala sio mzigo waweza tunzwa na ndugu wengine baba wakubwa au wasomi au wajomba au mashangazi au mababu au mabibj au mabinamu nk mleta mada atakuwa anatoka familia wasizojaliana ndio maana ana roho hii ya kikatili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…