Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
- #141
Magonjwa haya yanatisha sana mkuuLabda Cancer ya nywelee kijanaa...!! Bongo mpaka Dr akajua una cancer bhasi ukiishi zaidi ya miaka mitano mshukuru Mungu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Magonjwa haya yanatisha sana mkuuLabda Cancer ya nywelee kijanaa...!! Bongo mpaka Dr akajua una cancer bhasi ukiishi zaidi ya miaka mitano mshukuru Mungu.
Hii sina uhakika nayo. Ngoja tusubiri kusikia doctors watasemajeWatu wanafanyiwa chemo wanaishi zaidi ya miaka 10 wengi nawafahamu usiishi kwa kukariri .
Hapana mkuu...Kwani kaburini tunaenda na mali?
Basi kama tunaziacha tupiganie uhai mpaka mwisho, MUNGU ana njia zake za kutunza wasio na hatia maana hata yuo mtoto anaweza pata ugonjwa akihitaji kupiganiwa kama mtu mzima.Hapana mkuu...
Hii ya kusema kwamba Mungu atawapa tena licha ya kutoka kuwa na nyumba kisha kurudi kupanga chumba na sebule inahitaji mtu mwenye imani kubwa sana kama wale wazee wa kwenye biblia.Kwani kaburini tunaenda na mali? Pigania uhai hata kama utabakiwa na sifuri. Kuna watoto kibao wanazaliwa wazazi hawana nyumba na MUNGU huwatafutia njia.
Kwa sisi tunao amini Dini na ndiyo usawa huu, ni kosa kubwa sana kukata tamaa katika neema za Mola muumba. Sababu yeye ni muweza wa yote.Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.
Ndugu zangu Watanzania;
Kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa. Familia masikini/fukara kuuza nyumba yao ya pekee ni pigo kubwa sana kwa watoto wadogo.
Ninaandika haya nikijua fika ya kwamba hakuna idadi ya mali au pesa kinachoweza kulingana na uhai wa mwanadamu. Unakumbuka ajali ya MV Bukoba wewe? Unakumbuka ajali ya MV Spice kule Zanzibar?
Ni Watanzania wangapi walikufa katika ajali zile? Hivi wakati wa majanga yale uliwahi kusikia hata siku moja Watanzania wanalalamika kuhusiana na thamani ya zile meli?
Unajua gharama ya vyombo vile ni mamilioni ya pesa ngapi za Kitanzania? Licha ya kuwa ni pesa nyingi sana zilitumika katika kununua/kuunda vyombo vile Watanzania bado wakawa wanalilia roho za binadamu wenzao kwa maana kwamba hakuna cha kufananisha na uhai wa mwanadamu.
Hiyo ndio asili ya huruma ambayo Mungu ametupa sisi wanandamu. Familia zetu hizi masikini, mali tunazipata kwa tabu sana, ujenzi wa kuungaunga nyumba moja unajenga kwa kudunduliza miaka zaidi ya 9.
Baada ya ujenzi kukamilika, mnaishi miaka yenu 3, alafu ghafla mnasikia baba yenu mzazi anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ini au figo zote zimefeli anapaswa kupelekwa India kwa matibabu zaidi.
Ndugu wanajitahidi kuchangisha kwa jamaa na rafiki zao hapa na pale kiasi hakifikii pesa sahihi inajohitajika kuweza kukidhi gharama za matibabu hivyo wanaamua kuuza mali zao za thamani walizonazo kumpeleka baba yao nje ya nchi (India) kwa matibabu zaidi.
Matokeo yake baba anakufa, mzee wa miaka 69, na mali zote mmeuza. Unaikuta familia iliyotoka kupanga chumba na sembule kisha wakajikwamua kujenga wanarudi tena katika nyumba za kupanga na maisha ya kuomba omba.
Nimemua kuleta mada hii hapa baada ya kukutana na kijana mmoja jina lake ni ****** ambaye nilikuwa ninakaa nao Keko Juu mwaka 2011 ambaye baba yao alifariki mwaka 2014 kwa ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo.
Inasemekana kwamba mzee yule wa miaka 66 hakuwa na matumaini ya kupona, kulingana na taarifa ambazo mmoja wa ndugu yao wa karibu (baba mdogo) alipewa na daktari katika hospitali moja maarufu tu hapa Dar.
Kwa kuwa familia bado ilikuwa inampenda na kumthamini mzee wao wakaona ni bora wauze hata nyumba waliokuwa wanajenga huko Toa Ngoma njia ya Kongowe ili wampeleke baba yao huko India. Matokeo yake ndio kama haya. Wamepoteza vyote, baba pamoja na nyumba.
Mama ndio hivyo tena biashara za kuungaunga za akina mama lishe, dada zake wawili walizaa tu hapo nyumbani yaaani nilipoonana na huyu kijana (ni agemate na mimi) machozi yalitaka kunitoka.
Basi tu kwa kuwa na mimi mwenyewe ni Taxi Driver mlala hoi sina cha kumpa zaidi ya kusimuliana story za zamani tulipokuwa tunacheza mpira (cha ndimu) wote na kwenda kuogelea baharini kule Kurasini tulikuwa tunapaita ZAMCARGO au SAVA.
Ndugu zangu, kuna stage ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike tusizidishe umasikini katika familia.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Sawa mkuu...Kwa sisi tunao amini Dini na ndiyo usawa huu, ni kosa kubwa sana kukata tamaa katika neema za Mola muumba. Sababu yeye ni muweza wa yote.
Cha msingi ni kupambana mpaka nukta ya mwisho.
Mbona una imani kuwa ukimwacha mgonjwa afe ili nyumba ibaki aliyeachiwa nyumba hatakufa karibuni ila yeye na familia wataishi maisha bila kuhangaika na kodi? Kwani ni ww unayetoa pumzi?Hii ya kusema kwamba Mungu atawapa tena licha ya kutoka kuwa na nyumba kisha kurudi kupanga chumba na sebule inahitaji mtu mwenye imani kubwa sana kama wale wazee wa kwenye biblia.
Asante kwa busara zako mkuuKwa sisi tunao amini Dini na ndiyo usawa huu, ni kosa kubwa sana kukata tamaa katika neema za Mola muumba. Sababu yeye ni muweza wa yote.
Cha msingi ni kupambana mpaka nukta ya mwisho.
Mali hutafutwa kama hawakuwa nazo hapo mwanzo kisha wakawa nazo, kisha wakapoteza mali hizo, hilo si jambo baya tena uzuri zimetumika katika jitihada ya kuokoa maisha ya mtu wao, haina shida. Kwahiyo waendelee kupambana na wasikate tamaa, watapata tena na mambo yatakuwa sawa.
Mkuu, sipingani na hoja yako kwa maana ina mashiko na mantiki sana ndio maana nikasema inategemeana na imani ya mhusika/wahusika.Mbona una imani kuwa ukimwacha mgonjwa afe ili nyumba ibaki aliyeachiwa nyumba hatakufa karibuni ila yeye na familia wataishi maisha bila kuhangaika na kodi? Kwani ni ww unayetoa pumzi?
Ok mkuu... ila umaskini ni wa kuchukia sana, hata vifo vingi vinasabibishwa na umasikini.Mkuu, sipingani na hoja yako kwa maana ina mashiko na mantiki sana ndio maana nikasema inategemeana na imani ya mhusika/wahusika.
Umasikini ni adui wa uhai pamoja na maendeleo kwa ujumlaOk mkuu... ila umaskini ni wa kuchukia sana, hata vifo vingi vinasabibishwa na umasikini.
Hii ndio busara yenyewe mkuu...Na hata sisi tukiumwa tuache kuwa wabinafs umesha enjoy life san mpk 65 afu unaumwa na possibility ya kupona ni ndogo au hata ukipona utairudisha familia nyuma sana
Mgonjwa inabidi uwe na huruma na unaowaacha waambie tu ukwel mimi nitangulizen mbele ya haki kwa namn yeyote ile
Watoto wadogo wakiachwa bila pahala pa kuishi ni mzigo mzito sana kwa familiaNa hata sisi tukiumwa tuache kuwa wabinafs umesha enjoy life san mpk 65 afu unaumwa na possibility ya kupona ni ndogo au hata ukipona utairudisha familia nyuma sana
Mgonjwa inabidi uwe na huruma na unaowaacha waambie tu ukwel mimi nitangulizen mbele ya haki kwa namn yeyote ile
Kuumwa ni ibada na ikitokea tumeumwa kwa kiasi hicho bas tujaribu kuwafikiria na tunaowaacha watakuwa katika hali gan pind tukiwaacha
Doctor sio MunguKuna vitu vingine kwa sisi waafrika hufanyika kutokana na ujinga wetu. Sasa doctor kakwambia utakufa, mnalazimisha nini? Istoshe asilimia kubwa ndiyo uhamia kwa waganga wa kienyeji na wazee wa upako
Kazi ya doctor si kutamka mgonjwa atakufa ni kutibuKuna vitu vingine kwa sisi waafrika hufanyika kutokana na ujinga wetu. Sasa doctor kakwambia utakufa, mnalazimisha nini? Istoshe asilimia kubwa ndiyo uhamia kwa waganga wa kienyeji na wazee wa upako
Familia za kibwege ndio huwa mzigo ila familia wanaojaliana wala sio mzigo waweza tunzwa na ndugu wengine baba wakubwa au wasomi au wajomba au mashangazi au mababu au mabibj au mabinamu nk mleta mada atakuwa anatoka familia wasizojaliana ndio maana ana roho hii ya kikatiliWatoto wadogo wakiachwa bila pahala pa kuishi ni mzigo mzito sana kwa familia