Kuna hatua ugonjwa ukifika ni lazima busara itumike. Mnauza mali zote kulipia matibabu, ndugu anakufa kisha familia inabaki na umasikini wa kutupwa

Fanya ufanyalo lkn kufa utakufa kufa ni lazima kufa ni destur sasa inakiwekaje ktk ivo vitu na wakat lazima kila nafsi ionje maut
Kwa wakristo hatuamini kuwa kila nafsi itaonya Mauti you usemi ni uongo ni baadhi ndio wataonja mauti kwa mfano kwenye Biblia Henoko na Eliya hawakuonja mauti walipaa wazima wazima lakini pia mwisho wa dunia au kiyama kikifika sio watu wote kitawakuta wakiwa marehemu wengine kitawakuta wazima wa afya!!! Hawajaonja mauti wala kujua kaburi linafananaje
 
Basi kama tunaziacha tupiganie uhai mpaka mwisho, MUNGU ana njia zake za kutunza wasio na hatia maana hata yuo mtoto anaweza pata ugonjwa akihitaji kupiganiwa kama mtu mzima.
Mkono hujikuna pale unapofika. Tupiganie afya/uhai wa wapendwa wetu kadri ya hali zetu za uchumi zitakaporuhusu ila "busara" nayo itumike
 
Kwamba hiyo Nyumba isingeuzwa huyo Jamaa yako angekuwa hali afadhali?

Hiyo Nyumba ya familia ingemuingizia vipi kipato kama yeye hana shughuli inayomuingizia kipato?.
 
Kwamba hiyo Nyumba isingeuzwa huyo Jamaa yako angekuwa hali afadhali?

Hiyo Nyumba ya familia ingemuingizia vipi kipato kama yeye hana shughuli inayomuingizia kipato?.
Kuna watoto wadogo nadhani watakuwa darasa la tano au la sita wale kama sijakosea kwa maana ni muda kidogo umepita
 
Hivi mnauza kibanda kama hiki hata hayo matibabu kitachangia kiasi gani? na wanaobaki ndio kama huyu? Na mkiuza anaenda kuishi wapi?
 
Baada ya kuziacha wenyewe wapo au nao waliondoka....busara inayozungumzwa hapa ni hawa wanaobaki wanabaki katika khali gani...hakuna asiyempenda mgonjwa lakini pia wanaobaki.....hizo unazosema zinapita ndio tunazopambania tangu tunapoanza kuvuta pumzi mpaka tunaiacha....na baadae ukitafakari unagundua kama unakimbiza upepo....
 
Wanaobaki wapo hai na afya njema, watafute mali zao, tutafute hela na mali zetu binafsi zitulinde sisi. Siyo kuwalinda wanaobaki. Hapa utakuta mibaba na mimama mijitu mizima imelemaa na mali za wazazi!

Labda kama familia ni changa watoto wanasoma primary!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Nilichokiona kwenye hii mada ni kuwa kuna baadhi ya jamii humu sense ya community life tuliyozoea waafrika imeanza kuondoka kuwa mtu akifariki watoto wake hawatakuwa na pa kwenda!!!! ni kama vile hawana ndugu hawana baba mdogo au mkubwa ,Hawana shangazi wala mjomba .Hawana babu wala bibi .Hawana ndugu kabisa wa karibu wa ku wa care!!! Tumeingia kwenye maisha ya kizungu ambapo kila mtu ni yeye tu na maisha yake na wanawe!!!!

Ukisoma comments humu unajua kirahisi tu mtu anaishi maisha gani ni community life au ni yeye na wanawe tu!!!
 
Wanaobaki wapo hai na afya njema, watafute mali zao, tutafute hela na mali zetu binafsi zitulinde sisi. Siyo kuwalinda wanaobaki.
Watoto wadogo wa darasa la nne watawezaje kutafuta mali zao mkuu?...
 
Kuna magonjwa sawa unaweza kutumia busara Kama cancer

Ila ushawahi kujiuliza why wanapambana hvyo kumuweka hai mpendwa wao!!!

Kumpoteza mtu kusikie kwa wenzako tu
Ni mtihani mgumu na nadhani utamaduni wetu hatujaandaliwa kwa ajili ya mazingira kama hayo. Tatizo kubwa sana lilipo ni la wataalam wetu wa afya kutosema ukweli, unakuta mtu ameonekana kansa imesambaa mwili mzima unamdanganya akienda India/South atapona wakati sio kweli.
Kiukweli kuna magonjwa/matatizo yakikupata jikabizi kwa mungu na kubali matokeo, namuangaliaga yule jamaa sijui ni Mzanzibar au ambaye Makonda alitumia millions kumpeleka India lakini karudi kama alivyoenda, issue kama hizo za uti wa mgongo hata wazungu wanakuambia kabisa uwezekano wa kupona ni mdogo saana labda miujiza itokee lakini jamaa kadanganywa kaenda kutumia pesa ambazo wangeweza fanyia mambo mengine ya kurahisisha maisha yake yaliyobaki duniani.
 
Topic Kama hii inafaa uilete hapa ikiwa wewe mwenyewe ndio mhusika mkuu wa tukio
 
Ebwana mimi hiyo hitimisho yako huwa siipendi na hiyo style ya kurudia heading pia inachosha

msema kweli mpenzi wa MwenyeziMungu
 
Ebwana mimi hiyo hitimisho yako huwa siipendi na hiyo style ya kurudia heading pia inachosha

msema kweli mpenzi wa MwenyeziMungu
jamiiforums ina wanachama zaidi ya 500,000 hivyo siwezi kumfurahisha kila mtu.

Msema kweli mpenzi wa Mwenyezi Mungu
 
Topic Kama hii inafaa uilete hapa ikiwa wewe mwenyewe ndio mhusika mkuu wa tukio
Wengine tumeshapita huko, na shida ilikuwa maDr walikuwa wanadanganya kuwa mzee ana tatizo flani linalotibika lakini kwa pembeni wanawaambia watu baki kwamba huyu mzee hana muda mrefu, kansa imesambaa kila mahali. Kukawa na plan ya kwenda India, wakataka vipimo flani ambavyo ilibidi kwenda Muhimbili baada ya kama wiki nikawa na wasiwasi na hali ya mgonjwa maana alikuwa katika hali ambayo hawezi safiri mwenyewe, kumbana Dr mmoja akawa mkweli akasema huyu mzee ana prostate cancer na imeshakula organs zote na cha kufanya sasa nawapa dawa za kupunguza maumivu mrudisheni nyumbani akapumzike. Hakumaliza week 2 mzee akapumzika.
 
Poleni sana
 
nyumba imeuzwa wanaoishi ndani wakapatwa na mshtuko wa moyo au presha wakafariki na wao ,badala ya mtu mmoja wanafariki watu wawili au watatu..je ni sahihi.?.
 
Uhai ulikuwepo kabla ya binadamu kugundua pesa na nyumba,Mimi nitauza kila kitu kupigania uhai was mmpendwa wangu!

Haya mavitu niyakutafuta Ila uhai haununuliwi haijalishi nitabaki kwenye wakati gani nitanyanyuka na kupambana tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…