Wengine tumeshapita huko, na shida ilikuwa maDr walikuwa wanadanganya kuwa mzee ana tatizo flani linalotibika lakini kwa pembeni wanawaambia watu baki kwamba huyu mzee hana muda mrefu, kansa imesambaa kila mahali. Kukawa na plan ya kwenda India, wakataka vipimo flani ambavyo ilibidi kwenda Muhimbili baada ya kama wiki nikawa na wasiwasi na hali ya mgonjwa maana alikuwa katika hali ambayo hawezi safiri mwenyewe, kumbana Dr mmoja akawa mkweli akasema huyu mzee ana prostate cancer na imeshakula organs zote na cha kufanya sasa nawapa dawa za kupunguza maumivu mrudisheni nyumbani akapumzike. Hakumaliza week 2 mzee akapumzika.