Kuna hela naisikilizia

Kuna hela naisikilizia

MIGUGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
2,137
Reaction score
3,931
Naheshimu sana huu msemo"Kuna hela naisikilizia".Nashangaa watu wanaubeza na wanadharau pale wanapoambiwa.

Mtu anayesema hivi ina maana moyo unataka lakini pesa haipo kwa wakati huo kukamilisha utatuzi wa hiyo shida.Kuna vingi vinachangia.

Kila mtu akitimiza wajibu wake kwa wakati hili neno kuna hela nasikilizia litakuwa likionesha matumaini. Kama unadaiwa mlipe mtu yawezekana wewe mnachelewesha hivyo inabidi amwambie mtu mwingine "Kuna hela naisikilizia".

-Kama ni boss muongeze mfanyakazi wako mshahara ulioahidi kwa wakati.
-Mteja mlipe muuzaji kwa wakati.
-Mzazi mpe mwanao kwa wakati
-Serikali walipeni watu kwa wakati
-Makampuni lipeni kwa wakati
-Wazee wapeni vijana fursa.

Kwa ufupi heshimuni hustle za watu.Maana huu msemo "kuna hela naisikilizia"ni wakuonesha matumaini kwa sababu kuna watu wanawacheleweshea pesa zao ili kukamilisha mzunguko wa hela wapeni hela kwa wakati.
 
Ubaya wa kusikilizia hela ni kwamba hua hela haiji sasa ni bora uifate huko huko, halafu tangu lini hela ikasikiliziwa? Hela inatafutwa co kuisikilizia.
 
Ubaya wa kusikilizia hela ni kwamba hua hela haiji sasa ni bora uifate huko huko, halafu tangu lini hela ikasikiliziwa? Hela inatafutwa co kuisikilizia.
Sasa kama nimeweka mkeka na mechi haijaisha si ndio naisikilizia mzee?
 
Back
Top Bottom