DOKEZO Kuna hujuma kukwamisha kituo cha Misugusugu kufanya kazi?

DOKEZO Kuna hujuma kukwamisha kituo cha Misugusugu kufanya kazi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ningependa kuwauliza wizara ya Uchukuzi kupitia Waziri Bashungwa ni lini Kituo cha ukaguzi wa mizigo kilichopo kata ya Misugusugu mkoani Pwani kitahamia Vigwaza kuliko jengwa kituo kikubwa cha ukaguzi kupitia fedha za udhamini wa Bank ya Dunia?

Sababu kituo cha Misugusugu ni kama kipo kimtego wageni ambao sio wenyeji kuweza kujua kuwa maeneo hayo kuna kituo cha ukaguzi inakuwa ni kazi ngumu kwao sababu ni mala nyingi IT na Transit mbalimbali hujikuta wamepitiliza mpaka mizani ya Vigwaza au wakati mwingine mpaka Chalinze kutokana na kituo cha Misugusugu kuwa pebembezoni sana mwa barabara kuu ya Morogoro.

Kumemekuwapo na taarifa zinazo onyesha kuwa majengo yanayotumiwa na TRA pale misugusugu ni mali ya kigogo mmoja naye ndie anayekwamisha kituo cha ukaguzi Vigwaza kuweza kuanza kutoa huduma japo kimekamilika ila TANESCO wameshindwa kuweka huduma ya Umeme leo ni mwaka wa pili.
 
Back
Top Bottom