Kuna jamaa yangu alikua USAID akawa ananifungia vioo, leo kanitumia ujumbe kama nina mchongo wowote nimpasishie

Mtoa post nawe limbukeni na maskini tu ndio nini kumuanika mwanaume mwenzio huku kwenye forum.
 
Huna jamaa yoyote wa huko sema ni wivu tu ulikua unakusumbua sasa umeona fursa ya kuwasimanga.
 
mmmh binadamu kazi sana.
 
Sijaona tatizo la jamaa wako wa USAID.
Alijuaje kama jamaa anadharau?,alijuaje kama jamaa kamfungia vioo? .sio mtu anapiga simu muda wa kazi isipopokelewa unasema kakufungia vioo.

Mimi nilipomaliza chuo miaka mingi iliopita ,nilikuwa naona wenzangu kama wananifungia vioo sababu wamepata kazi nzuri na wengi cycle yangu walikuwa washapita hatua kubwa sana.
lakini nilipoanza kupata kiasi ambacho nimejaaliwa na Mungu nikaanza kuona ilikuwa ni bias tu , wengi walikuwa busy sana na majukumu mengi. familia za kiafrika akitoka mmoja tu basi ndugu jamaa marafiki ,ukoo wanadondokea huko.

Tujifunze kitu pia ,ukipata usidharau au kumfungia viooo aliepo nyuma yako

Ally Mohamed, Nairobi 18:00 EAT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…