Kuna kampuni zina laana, Hakuna mwajiriwa katoboa, Pesa haikai, matatizo kila kukicha

Kuna kampuni zina laana, Hakuna mwajiriwa katoboa, Pesa haikai, matatizo kila kukicha

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Kuna kampuni zingine unaweza kudhani zina laana.

Unakuta hakuna waajiriwa waliopiga hatua, wapo wenye hali zinazozidi kuwa mbaya, wenye nafuu wapo pale pale walipoanzia.

Yani unakuta kila alieajiriwa kawa kama mtumwa, shida hazikauki, nuksi kama zote, kufupista story sahau kuhusu maendeleo

Kila anaelipwa mshahara utadhani kuna tatizo lilikuwa linamsubiri apate pesa, Pesa haikai kufanya uwekezaji wala savings,

Nakumbuka kuna kampuni niliwahi kufanya kazi mwaka na nusu watu mule ndani wananuka madeni, kwenye story shida ndio maada kuu kila mtu ni gangwe wa kuelezea shida alizopitia, n.k.

Niliacha kazi hata waliponiambia wataniongezea mshahara kwa 20%, nilipoondoka nilistruggle kwa miezi kadhaa ila sehemu mpya niliyopata kazi nilianza kuona nuru ya maisha, niliweza kusave pesa kuanzisha biashara za nje mpaka nikafikia hatua ya kuacha kazi kusimamia miradi binafsi, sio mimi peke yangu ila co - workers wengi niliowahi kufanya nao kazi wanapiga hatua.
 
Njoo tuwekeze kwenye mbao mkuu acha kutumwa tumwa
Kila biashara ina elimu, ujuzi na changamoto tofauti, unaweza kuona mbao ni rahisi ila haipo hivyo kwa wengine, mimi nipo sekta ya usambazaji wa vifaa na vitabu mashuleni
 
Back
Top Bottom