Kuna kero za Muungano au Muungano ni kero?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Muungano ulioasisiwa na Karume na Nyerere ni tofauti sana na muungano tunaouona leo. Maana baada ya muda tayari tunawaza uwepo wa Tanganyika baada ya kuona uwepo wa Zanzibar.

Wakati awali Karume alikuwa makamu wa Rais, leo Zanzibar ina Rais kamili na ina makamu wako. Na hiki ndicho chanzo cha Zanzibar kudai uwepo wa kiti chake UN, na maeneo mengi wanaandika ni Semi autonomous State.

Kimsingi muungano unaifanya Tanzania kuwa nchi moja lakini utashangaa kwamba kuna mambo ni ya bara au visiwani ambayo tumeyaita mambo yasiyo ya muungano. Yaani badala ya kuwa na mambo ya kufanya kwa pamoja tumeanza kugawa kwamba haya yafanyike kwa utofauti. Hadi tunashindwa kuelewa kama Tanzania ni nchi yenye majimbo mawili au namna gani.

Kutokana na haya tumekuwa busy kutatua kero za muungano lakini kwa hali ilivyo, muungano ndio kero.

Hivyo naona malalamiko ya kero za muungano hayatoisha hadi siku tutakayovunja muungano au kufanya kila nchi ishinde mechi zake.

Nawasilisha.

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Nimekuwa niki analyze hili jambo kwa muda nimeona ni share na great thinkers

Kama Tanganyika ikirudi basi Zanzibar ina haki ya kurudisha mipaka ya 1886, Kilometa 16 ya ardhi kutoka kwenye fukwe za Bahari ya hindi, kuanzia Tanga,. Pangani, Bagamoyo, Dar es Salaam, Kilwa, Lindi, Mtwara, mpaka Mafia zinarudi Zanzibar, haya ni maeneo hata Nyerere alikuwa akijua lakini ilibidi itumike akili ya ziada.

Nyerere hakuwa mkamilifu lakini si haba alikuwa na uwezo mkubwa wa akili, Hakufanya maamuzi haya kwa kukurupuka kama wengi tunavyodhani, Maeneo hayo yana umuhimu mkubwa sana ingekuwa ni pigo kuyapoteza, Ni muhimu sana kiasi kwamba ilibidi yafanyike maamuzi ya kuifuta Tanganyika kuwe na Tanzania na bado tena Zanzibar wawe na Serikali yao kwa kiasi fulani, Ni kwamba tulikuwa kwenye tight spot ilibidi kila namna ifanyike kwa namna ya kidiplomasia ili mpango ukamilike kimya kimya na dunia ijue Zanzibar Haikulzimishwa bali imeridhia, Endapo ingetumika nguvu / mabavu kungekuwa na kelele nyingi za umoja wa mataifa kuirudishia Zanzibar ardhi yote.

1725578718021.png

1725579530364.png
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa aina yake lakini moja ya jambo jema walilofanya Nyerere na mzee Karume ni kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuwa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Marais waliofuata baada ya Nyerere ndio wamepwaya sana kuuenzi Muungano. Kulitakiwa kuwe na serikali moja tu ambayo ni ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Karume asingeweza kukubali aina hio ya muungano wa nchi moja

Ilibidi kumshawishi kidiplomasia aone kwamba atafaidika zaidi kwa Tanganyika kufutwe iungane na Zanzibar huku bado Zanzibar ikiendelea kuwa nchi yenye serikali yake, raisi wake, bunge lake, n.k.

Yote haya yalifanyika ili dunia ishuhudie Zanzibar haijalazimishwa bali imeridhia, Vinginevyo hali ingekuwa tofauti, Kungekuwa na hatari ya Oman na nchi nyingine kupata sababu ya kuisaidia Zanzibar kurudisha maeneo yake kwa njia ya vita.
 
Karume asingweza kukubali aina hio ya muungano wa nchi moja

Ilibidi kumshawishi Tanganyika ifutwe iungane na Zanzibar na pia Zanzibar iendelee kuwa nchi kwa kiasi fulani,

Yote haya yalifanyika ili dunia ishuhudie Zanzibar haijalazimishwa bali imeridhia, Vinginevyo hali ingekuwa tofauti.
Pamoja na hilo muungano ulitakiwa kufikia kuwa na serikali moja tu ambayo ni ya JMT.
 
Nimekuwa niki analyze hili jambo kwa muda nimeona ni share na great thinkers

Kama Tanganyika ikirudi basi Zanzibar ina haki ya kurudisha mipaka ya 1886, Kilometa 16 ya ardhi kutoka kwenye fukwe za Bahari ya hindi, kuanzia Tanga,. Pangani, Bagamoyo, Dar es Salaam, Kilwa, Lindi, Mtwara, mpaka Mafia zinarudi Zanzibar, haya ni maeneo hata Nyerere alikuwa akijua lakini ilibidi itumike akili ya ziada.

Nyerere hakuwa mkamilifu lakini si haba alikuwa na uwezo mkubwa wa akili, Hakufanya maamuzi haya kwa kukurupuka kama wengi tunavyodhani, Maeneo hayo yana umuhimu mkubwa sana ingekuwa ni pigo kuyapoteza, Ni muhimu sana kiasi kwamba ilibidi yafanyike maamuzi ya kuifuta Tanganyika kuwe na Tanzania na bado tena Zanzibar wawe na Serikali yao kwa kiasi fulani, Ni kwamba tulikuwa kwenye tight spot ilibidi kila namna ifanyike kwa namna ya kidiplomasia ili mpango ukamilike kimya kimya na dunia ijue Zanzibar Haikulzimishwa bali imeridhia, Endapo ingetumika nguvu / mabavu kungekuwa na kelele nyingi za umoja wa mataifa kuirudishia Zanzibar ardhi yote.

View attachment 3088278

View attachment 3088280
Kumbe kwenye bendera ya Tanganyika tumeongeza rangi ya blue bahari
 
VITENDO VYA UTEKAJI NA WATOTO KUPOTEA VINATUKWAZA MNO WATANZANI.

HILI NI TATIZO KUBWA SANA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA.
 
Muungano ulioasisiwa na Karume na Nyerere ni tofauti sana na muungano tunaouona leo. Maana baada ya muda tayari tunawaza uwepo wa Tanganyika baada ya kuona uwepo wa Zanzibar.

Wakati awali Karume alikuwa makamu wa Rais, leo Zanzibar ina Rais kamili na ina makamu wako. Na hiki ndicho chanzo cha Zanzibar kudai uwepo wa kiti chake UN, na maeneo mengi wanaandika ni Semi autonomous State.

Kimsingi muungano unaifanya Tanzania kuwa nchi moja lakini utashangaa kwamba kuna mambo ni ya bara au visiwani ambayo tumeyaita mambo yasiyo ya muungano. Yaani badala ya kuwa na mambo ya kufanya kwa pamoja tumeanza kugawa kwamba haya yafanyike kwa utofauti. Hadi tunashindwa kuelewa kama Tanzania ni nchi yenye majimbo mawili au namna gani.

Kutokana na haya tumekuwa busy kutatua kero za muungano lakini kwa hali ilivyo, muungano ndio kero.

Hivyo naona malalamiko ya kero za muungano hayatoisha hadi siku tutakayovunja muungano au kufanya kila nchi ishinde mechi zake.

Nawasilisha.
Kwa sasa naona kama Muungano hauna tija tena,,Watz Bara hawaruhusiwi kufanya kazi Visiwani, Watz Bara hawaruhusiwi kumiriki ardhi visiwani ila wao kwetu wanafanya kazi, wanamiriki ardhi,,angalia hata teuzi,hakuna mbara anateuliwa Zbr ila wazbr wanateuliwa kuja Bara so this is biased/one side union
 
VITENDO VYA UTEKAJI NA WATOTO KUPOTEA VINATUKWAZA MNO WATANZANI.

HILI NI TATIZO KUBWA SANA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA
.
Kama una kitu nakielewa toka kwako inahitaji jicho la tatu kukuelewa, yaani muungano vs kutekwa na kupotea kwa watoto, hapo ukiunganisha dots utaelewa kwani kwasasa muungano vinahusiana na ................, (trust no one but yourself), the end result is human herding
 
Muungano ulioasisiwa na Karume na Nyerere ni tofauti sana na muungano tunaouona leo.
Hakuna tofauti tokea kuundwa kwake mambo ya msingi yapo vilvile.
Wakati awali Karume alikuwa makamu wa Rais, leo Zanzibar ina Rais kamili na ina makamu wako.
Huenda umesahau. Karume alikuwa, tokea mwanzo wa kuundwa mungano, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Wakati huohuo alikuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa JMT.
Kimsingi muungano unaifanya Tanzania kuwa nchi moja lakini utashangaa kwamba kuna mambo ni ya bara au visiwani ambayo tumeyaita mambo yasiyo ya muungano.
Ndivyo ilivyokuwa tokea kuundwa kwa muungano huu mwaka 1964. Angalia "the Act of the Union" ya mwaka 1964 na "Articles of Union" ya mwaka huohuo.
lakini kwa hali ilivyo, muungano ndio kero.
Haya ni maoni yako. Una haki ya maoni
Hivyo naona malalamiko ya kero za muungano hayatoisha hadi siku tutakayovunja muungano au kufanya kila nchi ishinde mechi zake.
Ni kweli kwa sababu bado tunaishi. Tujitahidi kila kwenye kero tuziondoe. Anayeota kuuuvunja muungano wacha aote na ikiwezekana atekeleze ndoto yake ili kuondoa kero.

Sisi tunaangalia kwa makini.
 
Huu Muungano ufe tu unakera sana na wale wanaotisha kwamba sijui Muungano ukivunjika mipaka itarudi ya miaka ya 1886 waache uzuzu,mbona kabla hatujaungana hiyo mipaka mnayosema haikutumika? Kama vipi waamie huko Zanzibar haiwezekani watu mamilioni tutawaliwe na kijiwilaya kwa kisingizio cha Muungano.
 
Huu Muungano ufe tu unakera na wale wanaotisha kwamba sijui Muungano ukivunjika mipaka itarudi ya miaka ya 1886 waache uzuzu,mbona kabla hatujaungana hiyo mipaka mnayosema haikutumika? Kama vipi waamie huko Zanzibar haiwezekani watu mamilioni tutawaliwe na kijiwilaya kwa kisingizio cha Muungano.
Hivi muungano ukifa CCM itabaki Zanzibar au bara?😁
 
Kama Tanganyika ikirudi basi Zanzibar ina haki ya kurudisha mipaka ya 1886, Kilometa 16 ya ardhi kutoka kwenye fukwe za Bahari ya hindi, kuanzia Tanga,. Pangani, Bagamoyo, Dar es Salaam, Kilwa, Lindi, Mtwara, mpaka Mafia zinarudi Zanzibar,

View attachment 3088278

View attachment 3088280
Hii 16km wide coastal strip haikuwa sehemu ya Zanzibar, bali sultan wa Zanzibar, mu-Oman ambaye alikuwa anawatawala Zanzibar kimabavu na hatimaye alifurushwa, ndiye alikuwa anadai ni mali yake. Siku muungano huu magumashi ukivujika, mpaka wa nchi hizi Tanganyika na Zanzibar utakuwa baharini halfway btn them.
 
Back
Top Bottom