Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Nimeona clip, mkuu wa wilaya wa Ubungo anavyoangaika na vitu vya ovyo utafikiri wilaya yake ya Ubungo wananchi wake wanatatuliwa na matatizo lukuki zinazowakabili. Niliwahi kwenda sehemu moja inaitwa Kisopwa kupitia barabara ya Kifuru kwenda hadi Vibula aisee barabara ni mbovu sana unaweza sema upo mkoani vijijini huko na kwa asilimia kubwa wilaya ya Ubungo ina barabara mbovu mno, swala la maji na afya bado ni changamoto.
Tuachane na hilo, twende kwenye hii mbinu anayotumia huyu mkuu wa wilaya ya Ubungo.
Kufanya ukaguzi kwenye vyumba wanavyolala watu kwa lengo la kuangalia kama umelala na mwanamke au kama kuna mwanamke yupo ndani sio sawa kabisa. Sio kosa kufanya inspection kwenye lodge ila unafanya inspection kwa lengo lipi? Na kithibiti ni kipi?
Nakumbuka niliwahi kulala lodge moja Njombe ila usiku wa saa nane waliingia askari polisi kwenye hiyo lodge kwaajili ya kufanya ukaguzi, ule ukaguzi ulikuwa ni sahihi kwavile unaulizwa maswali ya msingi kisha unapekuliwa kwenye begi lako na chumbani unapolala kama kuna kitu unacho ambacho ni kosa kisheria kuwa nacho/nayo hiko kinaitwa kithibiti.
Sasa huyu mkuu wa wilaya na mapolisi wao wanafanya vitu kitoto sana na anamdharirisha hadi aliyemteua.
Unaingia lodge kisha unalazimisha watu waliopo ndani ya chumba atoke huku analazimishwa aiangalie camera, huo si ni udhalilishaji? Hakuna uwakika kama huyo mtu ni mmoja wa muhusika au lah lakini analazimishwa aonekane kwenye camera.
Ile ni lodge na huenda kuna watu wengine wanatoka mikoani kwenda kupumzika hapo, au kuna watu wengine wanaenda na wapenzi wao hspo kwa faragha. Pengine wao wamewakariri sura au majina ya wanawake wanaofanya hiyo biashara hapo lakini mtu anayetumiwa kuwa ni mteja ana uwezo wa kukataa na kusema huyo ni mpenzi wake na hajaja kwa mauziano.
Mwisho hao wadada waliokamatwa wakiwa vyumbani kithibiti chao kuwa ni wanauza miili ni kipi?
Kuna fidia nzuri sana hapo kwa kufungua kesi ya udhalilishaji kama mmoja wa hao watu waliokamatwa wakiwa vyumbani endapo atapata mwanasheria mzuri.
Pia soma:

- Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo ,Mh Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni Malaya ?
- Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?
- Mkuu wa Wilaya ya Ubungo adhamiria kutokomeza biashara ya ukahaba