Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) (kwa sasa jina linawekwa kapuni) anatajwa kuvuruga mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge wa Jimbo la Ulanga, Morogoro.
Taarifa ndani ya CCM Mkoani Morogoro, zinaeleza kuwa Kigogo huyo ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini, aliteuliwa kusimamia vikao vya mchujo mkoani humo.
Inaelezwa baada ya figisu zilizotokea kwenye vikao vya mchujo ngazi ya wilaya, Kamati Kuu (MCC) ya CCM, iliteua na kuwaelekeza wajumbe wake kwenda mikoani kusimamia mchakato wa mchujo ngazi ya mkoa ambapo Kigogo aliteuliwa kusimamia Mkoa wa Morogoro.
Chanzo cha taarifa kinaeleza "Wajumbe wa Kamati Kuu (MCC), wote walisambazwa mikoani kusimamia vikao vya mchujo ngazi ya mkoa na ASAS aliteuliwa kwenda kusimamia mkoa wa Morogoro."
Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa Kigogo aliingilia kati uteuzi wa wagombea Ubunge Jimbo la Ulanga kwa sababu ya maslahi binafsi.
Taarifa za ndani zinadai kuwa vikao vya mchujo Mkoani Morogoro, vilipendekeza na kukubaliana kwa pamoja kuwa jina la Mgombea fulani amekosa vigezo kwa sababu ya tuhuma za rushwa zinazomkabili, hivyo amekiuka maadili, lakini Kigogo alihakikisha jina hilo linapitishwa kwenda kwenye vikao vya juu vya uteuzi ngazi ya taifa.
Jambo hili limezua hali ya sintofahamu kwenye Vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa. Hata, hivyo baadhi ya taarifa za kwenye mitandao ya Kijamii zinaonesha kuwa Kigogo ana ubia na mwajina wake anayefanana naye jina.
Duru za siasa zinaeleza kuwa Kigogo alitumia nguvu kubwa kuhakikisha mgombea huyo anapenya kwa kile kilichoelezwa kwamba wana uhusiano wa kibiashara na wadau wengine wenye ushawishi na siasa za hapa nchini.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo Kigogo alisema kwa nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati (MCC) na heshima aliyopewa na Rais hawezi kujiingiza kwenye siasa za aina hiyo.