DOKEZO Kuna kijiji wilaya ya Magu wageni wanaoingia kuishi kama wapangaji kulipa fedha za kiingilio kiasi cha shilingi 36,000 ndipo usajiliwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
 

Attachments

  • IMG-20250209-WA0004.jpg
    183.7 KB · Views: 3
Utaratibu mzuri sana huo waulete na huku mbagala[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Uko sawa, kuna mwamba mmoja mahali fulani aligoma hadi kwenda kushitakibkisa kaambiwa kutoa kiingilio tsh 20000/= na alikuwa na duka lake,jamii ikasema haijamzuia kuishi ila ni utaratibu tu,baada ya kama miaka 2 akavamiwa na wezi akapiga mwano lakini hakuna mtubaliamka hata mmoja wezi wakamwibia kama 13mls na wakawajeruhi ,kesho yake police wanakuja hakuna hata mtu mmoja pale eneo la tukio baada ya watu kukusanywa na kuulizwa kwa nn hawajaenda kusaidia wakasema huyo sio mwenzetu
 
Katiba ya inchi inasemaje kuhusu hilo? Ni kijiji gani?
 
Mimi naona ni sawaa tuu,and kama umeona ni kubwaa sio lazima uishi kijiji hicho Mkuuu

La pili wewe kijiji umekikuta kina huduma za kijamii ,hujui wamefikaje hapooo ,unataka kuwa chawaa ufaidi tuu Hapana ,kabisaaa Mkuuu,Kuwa muungwanaa mkuu pesa hiyo ni kidogo lipa upate uwanachama wa kijiji chetuuu,

Na usihangaike bure kutafuta mamlaka hapa maana hutofanikiwa mkuuu,
 
Wasukuma kumbe ni wangese ivyo.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Mkuu pole Kwa changamoto hiyo,ila Kwa uzoefu wangu wa kuishi Kanda ya ziwa hiyo pesa ni kiingilio Cha nzengo(umoja wa wakazi wa eneo husika kushirikiana Kwenye shida na raha).
Ulitakiwa kuhoji Kwa mwenyekiti au kuuliza wenyeji wakufahamishe zaidi.
 
Sahihi. Ni hiyari ila siku ukipatwa na jambo hapo ndipo utaona jamaa Wana roho mbayaa.
 
By law so lipa haina shida
 
Ni sawa ni utaratibu wao yafaa ulipe
 
Toa iyo hela tu 36k nayo ni ya kulalamikia serikali.
Ukute iyo ni ulinzi shirikishi.
Mademu na Bia mnatoa hela kiulaini ila apo mnataka serikali iwasaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…