A
Anonymous
Guest
Asalamu Alaikum ndugu,
Naomba muongozo kutoka kwa wahusika, hasa Kikosi cha Jeshi la Polisi Kitengo cha Barabarani na viongozi wengine.
Hapa mjini (Kata ya Sahara, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza) kuna kikundi cha watu takribani 10 wamejitokeza wakijihusisha na masuala ya madereva bajaji, kinakamata Bajaj kwa madai ya kupaki vibaya na kutoza faini ya Tsh. 22,000, lakini wahusika hawatoi risiti yoyote.
Wanasema wanafanya kazi kwa niaba ya Jeshi la Polisi Tanzania, jambo linaloleta sintofahamu. Tayari wamekamata Bajaj nyingi, na hali hii inaleta malalamiko na kuonekana kama ni uonevu.
Nataka kujua hawa watu wanapata wapi nguvu za kunyanyasa wadereva wa Bajaj jijini Mwanza halafu Jeshi la Polisi lipo kimya na kuna baadhi ya Polisi wanashirikiana nao kutoza hizo pesa, yaani Bajaj moja inaweza kukatwa 22,000 hata mara tano kwa siku na ukikataa wanachukua chombo wanapataka kukifungia, Halmashauri ya Jiji la Mwanza hawa watu wapo juu ya Waziri Mkuu?
Ufafanuzi wa Polisi ~ Jeshi la Polisi: Tunachunguza taarifa za kikundi kukamata madereva Bajaj Mwanza