Kuna kitu CCM wanakilinda kwa jasho na damu ambacho hatukijui

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
25,522
Reaction score
40,795
Kuna Siri CCM inaficha watanzania na ambayo itakuja kutuumiza au kuumiza vizazi vijavyo. Kuna kitu CCM inakilinda kwa jasho na damu, ni kitu Gani hiki?. Kwa fikra zangu za kawaida sidhani kama ni madaraka. Kuna kitu Zaidi ya hapo.

CCM wapo tayari kummiminia risasi raia Tena kwenye maeneo ya serikali ya CCM. CCM wapo tayari Kumfukuza Makamu wa Rais kisa tu kahoji kuhusu Katiba mpya. CCM wapo tayari kuua Raia wa Tanzania kisa wanataka mageuzi ya mfumo wa uchaguzi. CCM wapo tayari kubambikiza kesi za uhaini na ugaidi kwa watu wasio na hatia.

Lazima tujiulize Kuna Nini CCM wanakipigania hivi hadi kuona uhai wa watanzania hauna maana?. Jibu ni kwamba CCM wanalinda kitu Zaidi ya madaraka, wanalinda madhabahu yao. Ambapo siku madhabahu hiyo ikiwekwa wazi au ikipungua nguvu, watanzania watashuhudia vitu vya ajabu kiasi kwamba hawataamini wanayoyaona. Mambo ya ajabu yatatokea. Ulishawahi kuuliza kwanini CCM wanahangaika na CHADEMA mpaka wanatumia nguvu za ziada? Umewahi kujiuliza kwanini CCM inahangaika na Lissu? Mpaka kuamua kumpiga risasi na Sasa kesi ya uhaini ili anyongwe?. Jibu ni kwamba wametumwa na madhabahu yao maana inaona ya kesho na imegundua Lissu ana nguvu ambayo isipochungwa itaiathiri hiyo madhabahu huko mbeleni.

Hivyo CCM inaona Bora ilinde madhabahu yake ambayo ndio inaongoza Tanzania kwa Sasa, hata kwa gharama ya kuua watanzania. Maana nguvu ya madhabahu hiyo ya CCM ni kubwa kuliko mauaji wanayofanya. Maana madhabahu yao ikiishiwa nguvu Tanzania haitakalika hata kidogo, Siri nyingi zitakuwa wazi.

Suluhisho liliopo ni kupata madhabahu nyingine safi itakayopambana na madhabahu ya CCM. Kwa sababu madhabahu ya CCM ni chafu yenye Giza madhabahu ya kushindana nayo lazima iwe ni safi na yenye Nuru. Hapo ujanja wa CCM utaisha.

CHADEMA fanyieni kazi hili jambo. Tengenezeni madhabahu ya CHADEMA yenye usafi na Nuru ndipo mtaiweza CCM.
 
CCM ndiye shetani mwenyewe.
 
Madaraka hamna kingine.
 
Gentleman,
CCM ina wajibu mzito na mkubwa moja tu kwa taifa hili, nao ni
kulinda dhamana ya umma iliyopewa CCM na waTanzania kwa zaidi ya 90%, na dhamana hiyo ni kulinda umoja, amani na usalama wa waTanzania wote kwa mujibu wa katiba, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania wote. Full stop.

Mengine ni porojo na upotoshaji mtupu gentleman🐒
 
Unadhani wao ni wajinga kiasi kwamba wasijue siku wakikubali kuondoka madarani ndio siku wataanza kuishi maisha ya dhiki wao na vizazi vyao mpaka Kiama?

Maovu walioyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya haitatokea hata siku Moja wakubali kuachia madaraka kwa hiali. That's the point, hamna madhabahu wala nini
 
Wakitaka kujimaliza wamnyonge Lissu tu.
 
WANALINDA MASLAHI YAO NA VIZAZI VYAO TU. NI GENGE.
 
Yeah ...huwa wanajua kabisa litakalowakuta wao na associates wao . Kuna jamaa ni kama alinidokeza mbogamboga huwa mpaka wanaajiri makampuni ya nje katika kukifanyia chama chao tathmini na research mbalimbali ili kujua authenticity yao kwa Tanzania japo Sina uhakika na hilo
We ogopa kwamba mpaka senior military officers na wakubwa wengine kwenye maswala ya ulinzi wanafuatiliwa mienendo yao , unategemea nini? Ccm wanajua kabisa na wanajifunza yanayotokea Duniani kuanzia Madagascar mpaka west Africa huko ,hivyo lazima wachukue all possible precautionary measures ili ku maintain...
NB: Credit kwa mchina 😎🫢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…