Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 7,875
- 12,665
Inatokea watanzania tumeamua kwa pamoja kuwa wafugaji na katika ufugaji huo tukaamua kwa umoja wetu tufuge wanyama wawili tu, NGAMIA na NGURUWE. Na kwakuwa kuna uhaba wa malisho tukaona ni vyema wanyama hawa tukawalisha kwa msimu mmoja mmoja ili kuleta usawa baina ya wanyama hawa na kupata faida kubwa kama taifa
Sasa suala linakuja kuwa unapofika msimu wa malisho kwa NGURUWE tunaunganika kwa pamoja kama tulivyokubaliana kumlisha na kumnenepesha hadi msimu uishe na kweli atanenepa na mavuno tukapata makubwa bila hasara(changamoto) yoyote. Lakini ikija zamu ya NGAMIA mambo huanza kubadilika na kudhorotesha malisho, majani hayatamwagiliwa vizuri na wakati mwingine kufyekwa kabisa ili NGAMIA asishibe hatimae mavuno yanapatikana ila kwa tabu sana
Hili suala lazima tuliangalie kama tumeamua kufuga tufuge kama ufugaji umetushinda tuache mwenye kuelewa ameelewa
Ahsanteni