Kwanza Ahsantee kwa kuwa mstarabu na mtu mwenye sifa za kuitwa msomi.!
Niseme ukweli ambao huenda hujui au wakati mwingine unaufahamu toka muda mrefu. Ni kwamba, wanafunzi wanaodahiliwa kwenye vyuo vya binafsi ni mchanganyiko wa Mawe na Mchanga.! Namaanisha hili, vyuo vya watu au mashirika binafsi zaidi vimejikita kwenye kupata idadi kubwa ya wanafunzi ambao kwenye suala la vigezo hawajali sana ili mradi tu huyu mtoto ana D tatu katika masomo matatu .. Physics, Chemistry na Biology. Na kwa wafamasia, ndio wamekua cheap sana kwenye upande wa vigezo na utakuta vyuo vingi sana sasa hivi utakuta idadi ya wanafunzi wanaosoma famasi ni wengi mnoo kuliko kada zingine kwa sababu tu wao hata ile D ya physics hawaijali sana hata awe alipata F somo la hesabu.
Kwa vigezo hivyo, vyuo vya serikali vinachukuaga zile grade nzuri na kuacha wale wengine waliokosa huko serikalini kukimbilia vyuo vya Binafsi. Sasa ukija kuwaangalia hawa wanafunzi ambao hawajafaulu hesabu O level nafasi yao ya kufanya vizuri huku Elimu ya kati ni mdogo sana. Kwa mfano, course ya famasi kuna mahesabu yao wafamasia wanayo kwa mtu ambaye hesabu hakupata alama nzuri au hakuwa vizuri tu O level analiwa kichwa.
Na kufeli kwa wanafunzi wengi wanafeli kwa kutojali masomo, kujiamini sana na kuacha kusoma wakijua watapata Gaka na watachomoa.
Kingine, NACTE wanapaswa wajitahidi sana kuzifuatilia hizo A zinazopatikana vyuoni kama ni halali. Wengi wanapewa tu na walimu wao ili kuwafurahisha Mabosi wao au Waajili wa kwa Alama A hewa ambazo zikiingizwa kwenye chumba cha mtihani ambao haukuvuja zinageuka kuwa C na D. Waalimu wanafundisha mzee Baba..! Na kuacha hiyo kuna mafunzo maalumu yaitwayo Teaching methodology wanapatiwa walimu.
Nitarudi tena Mkuu Ahsantee [emoji1545]