Kuna kitu hakipo sawa

Ngengemkenilomolomo

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
270
Reaction score
450
Wakuu
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la viongozi kutoa kauli za kutisha, kuogofya na kutia mashaka lakini ajabu ni kwamba hawachukuliwi hatua si kwenye vyama vyao wala Serikali wanayoiwakilisha.

Hii inatia mashaka na kutoa ishara kwamba kwa pamoja wameshajua udhaifu wa dereva wa gari kwahiyo hawaogopi chochote maana wanajua hana uwezo wa kuwakemea wala kuwachukulia hatua.

Na kwakua dereva bado anataman kuendesha gari basi anawaacha wajimwaye mwaye maana wamemuhakikishia seat ya dereva haitokaliwa na mtu mwingine isipokuwa yeye no mara waa
Kinachoniuma zaidi ni kwamba alosema tutamkumbuka speed ya kumkumbuka imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Maana wale wale alowakataa yeye ndio hawa hawa wanaotoa kauli za kuumiza na kukandamiza wananchi. Natamani sana ufanyike muujiza katika lile box la twenty twenty five kwa mara ya kwanza katika historia tuondoe nguzo ya mkoloni lakini bahati mbaya ni kwamba refa ndio anayepanga matokeo.

Watu wa hali ya chini wanateseka, wanaumia, wanalia lakini hakuna anaejali, mbuzi wote wanakula
Kwa udhaifu wa mchungaji.
 
Ni uongozi uliofitinika unaoogopana kwa maslahi yao wenyewe.
 
Dereva anasimangwa ni aliambiwa asiondoe marufuku ya mikutano ya vyama vya siasa akakaidi...Ripoti mezani inaonyesha shughuli ni pevu ushindi wa bwelele haupo anawaambia wapige kazi kitu wasichokimudu sasa wanaona liwalo na liwe....Hata sterling hayuko sawa,anapiga mipasho tu...mwangalie huko Katavi na Rukwa hana la maana,hana utatuzi wa kero zaidi ni kijisifu na kutangaza kilichofanyika kama vile ni hakuna mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…