Kuna kitu sijakielewa kwa dada zetu hapa Tanzania

Kuna kitu sijakielewa kwa dada zetu hapa Tanzania

Ndugu yangu, siku hizi mapenzi yamegeuzwa biashara kwa asilimia kubwa
Ni kweli ila hata biashara wanapaswa kutumia akili kidogo!
Haiwezekani ndani ya siku mbili au week ukatangaza njaa ya Kila aina na kibaya mwingine anakwambia yupo na wazazi!!
 
yaani hii kitu nimeshindwa kuielewa kabisa kwa dada zangu na hapa Haina mwajiriwa Wala mdangaji, na naona kwa Sasa ni kwa Rika zote!
Inakuwaje utongozwe na ndani ya siku mbili Kila shida iliyopo duniani umwambie aliyekutongoza, hivi atawaza mapenzi nawe au shida ulizokuwa Nazo na hapo hapo unataka kukojozwa,
Au yananikuta Mimi tu Nini?
#Bakinahamuzako
 
Ni vile tu umejiweka kimkakati Mkuu, wewe usiangaike na mwanamke utajionea maajabu sana.

Dawa ya mwanamke ni kutoangaika naye, wewe kuwa bize na mambi yako, tengeneza pesa yako itumie wewe na familia/marafiki zako kifupi jipende.

Ukizijua tabia za paka umemjua mwanamke.
Sure
 
Tafuta tu hela ndugu yangu acha kulalamika hizo shida ni za kawaida au ulidhani ukimtongoza mwanamke akakubali imeisha hukujua kama kuna kumpa hela😁😁
 
Kwasasa wanawake wana akili sana,sie wanaume bado tunawaza eti wanapenda mapenzi kumbe wenzetu walishahama huko siku nyingi sahv wao wanataka pesa tu

Kuna mwanamke mmoja mzur sana,nilkuwa namuona kila mara nikawa nampotezea maana kwa jinsi siku hv walivyo machuma ulete hadi nawaogopa

Sasa kuna madogo wanaonisaidia kazi wakawa mara nyingi wananishauri niwe nae,wakawa wanamsifia kwa uzuri wake na tabia,kimwonekano huyo demu ni mzuri kweli afu mpole na hana marafiki kabisa

Zimepita siku nyingi sana tukawa tunaonana nampotezea,siku moja nikakutana nae uzalendo ukanishinda nikaamua nimsimamishe,nikachukua namba,mawasiliano yakaanza kwa speed ya ajabu,demu anatuma sms kila mara,tunachat mpaka saa 6 usiku,sijawah kuwa na demu wa kuchat namna hii hapo before,yaan mpaka nikajilaumu kwann nilkuwa najichelewesha

Siku moja nkamtoa out dem akaja kapendeza kinoma mpaka wanawake wenzie wanamtamani,tukapga story nying sana,dem ananiambia ametokea kunipenda sana ndani ya muda mfupi pamoja na kumwambia kuwa nimeoa tayar

Huyu demu aliwah kuolewa na akazaa watoto wawili,aliachika baada ya kwenda kwao kusalimia mama ake alikuwa mgonjwa,alivyotaka kurudi kwake mumewe akamtumia sms kuwa usije na atafute mwanaume mwingine wa kuwa nae na jamaa likaja mpaka kwao likachukua watoto,ndo akawa ameachwa hivyo

Yaan kilivyo kipole hadi nikawa nashangaa jamaa ilikuwaje hadi akamkataa kwa namna ile,basi penzi letu likaendelea kwa speed ya hatar,demu anatuma tu ma sms ya kuonesha kazimika balaa na mimi,ila demu mwenyew anajishungulisha sana na akaniomba nisije nikamuomba tunda haraka maana kuna wanaume aliachana nao haraka kwasababu ya kutaka tunda haraka,ananiambia hivyo ili kuniwahi maana ananipenda sana asije akanipoteza na mim nikamwambia hilo asiwe na shaka nalo

Ni mwanamke alieonekana yaan kama hela yangu haihitaji kabisa,hata nikimpa hela mfano 10,000 anasema acha tu nakuingiza kwenye matumizi ambayo ulikuwa hujayapangilia,basi kidume nikajiona nimepata mwanamke haswa yaan hana shida na hela yangu

Kumbe bhana alikuwa ananivuta mdogo mdogo,siku moja ananitumia sms nimuazimishe laki 1 baada ya wiki atanirudishia,nikatafakari sana ila nimeamua nimpe nione yatakayojiri,hata hivyo huwa napenda kuona na kuwasaidia wanawake wapambanaji,kwa kweli kwasasa nimeamini hawa wenzetu sio wa mchezo mchezo hawana time ya ujinga ni pesa tu.
 
Mambo yao waachie wenyewe, yasikuumize kichwa...
 
Hivi hiyo research yako umeifanya kwa wangapi hadi uje na hiyo conclusion kwamba "wanawake " tena umesema rika zote wanapenda pesa? Hamna wastaarabu wanaojitafutia pesa zao wenyewe? Why umegeneralize?

Kingine inategemea wewe mwanaume umeanza vipi kumtongoza mdada wa watu, kuna baadhi yenu mnaanza kwa sifa na kujionesha unapesa, yaani kama unatanguliza kumwonyesha una pesa na siyo upendo, hii inapelekea mdada aone kama kwako hamna upendo ni pesa tu.

Pia mtu kukuomba pesa sana siyo dalili nzuri, yaani ni mbinu ya kukukimbiza ikiwa hakupendi na unamng'ang'ania anaona bora akutangazie shida zake hadi ukimbie mwenyewe.

Kwa sisi wadada kama unampenda mtu na una malengo naye trust me huwezi kumsumbua kumuomba omba hela yaani unakua na huruma na pesa ya mwenzi wako.
So jichunguze na ubadilike mkuu,wadada wastaarabu wapo wengi tu.
 
Nimekusoma na Nina amini wapo ila Wachache sana,
Hilo la mwanamke akikuomba Hela hovyo hakupendi linaweza kuwa la ukweli kabisa!
 
Tafuta tu hela ndugu yangu acha kulalamika hizo shida ni za kawaida au ulidhani ukimtongoza mwanamke akakubali imeisha hukujua kama kuna kumpa hela😁😁
Kumuhudumia mwanamke Hilo halina shida ila Kuna mazingira unaombwa Hela mpaka unashangaa huu bila kuwa na mimi alikuwa anaishi vipi
 
Nimekusoma na Nina amini wapo ila Wachache sana,
Hilo la mwanamke akikuomba Hela hovyo hakupendi linaweza kuwa la ukweli kabisa!
Ni kweli mkuu kama mtu hakupendi anakupiga vizinga hadi ukimbie then atakupa sababu kwamba ulikimbia mwenyewe na siyo yeye kukukataa. Mbinu hiyo inafanya kazi, sorry to tell you this ila ndiyo ukweli
 
Ni kweli mkuu kama mtu hakupendi anakupiga vizinga hadi ukimbie then atakupa sababu kwamba ulikimbia mwenyewe na siyo yeye kukukataa. Mbinu hiyo inafanya kazi, sorry to tell you this ila ndiyo ukweli
Nimekuelewa sana, ila hata kama mtu ana shida kweli basi apunguze haraka ya kuzitangaza shida zake!
 
Nimekuelewa sana, ila hata kama mtu ana shida kweli basi apunguze haraka ya kuzitangaza shida zake!
Inategemea na umemuendeaje , ukimuendea kama una pesa sana hapo hapo nywele zinafumuka(hela ya saloon) , gas home inaisha, na kodi inaisha hapo hapo😂😂
 
Back
Top Bottom