Kwasasa wanawake wana akili sana,sie wanaume bado tunawaza eti wanapenda mapenzi kumbe wenzetu walishahama huko siku nyingi sahv wao wanataka pesa tu
Kuna mwanamke mmoja mzur sana,nilkuwa namuona kila mara nikawa nampotezea maana kwa jinsi siku hv walivyo machuma ulete hadi nawaogopa
Sasa kuna madogo wanaonisaidia kazi wakawa mara nyingi wananishauri niwe nae,wakawa wanamsifia kwa uzuri wake na tabia,kimwonekano huyo demu ni mzuri kweli afu mpole na hana marafiki kabisa
Zimepita siku nyingi sana tukawa tunaonana nampotezea,siku moja nikakutana nae uzalendo ukanishinda nikaamua nimsimamishe,nikachukua namba,mawasiliano yakaanza kwa speed ya ajabu,demu anatuma sms kila mara,tunachat mpaka saa 6 usiku,sijawah kuwa na demu wa kuchat namna hii hapo before,yaan mpaka nikajilaumu kwann nilkuwa najichelewesha
Siku moja nkamtoa out dem akaja kapendeza kinoma mpaka wanawake wenzie wanamtamani,tukapga story nying sana,dem ananiambia ametokea kunipenda sana ndani ya muda mfupi pamoja na kumwambia kuwa nimeoa tayar
Huyu demu aliwah kuolewa na akazaa watoto wawili,aliachika baada ya kwenda kwao kusalimia mama ake alikuwa mgonjwa,alivyotaka kurudi kwake mumewe akamtumia sms kuwa usije na atafute mwanaume mwingine wa kuwa nae na jamaa likaja mpaka kwao likachukua watoto,ndo akawa ameachwa hivyo
Yaan kilivyo kipole hadi nikawa nashangaa jamaa ilikuwaje hadi akamkataa kwa namna ile,basi penzi letu likaendelea kwa speed ya hatar,demu anatuma tu ma sms ya kuonesha kazimika balaa na mimi,ila demu mwenyew anajishungulisha sana na akaniomba nisije nikamuomba tunda haraka maana kuna wanaume aliachana nao haraka kwasababu ya kutaka tunda haraka,ananiambia hivyo ili kuniwahi maana ananipenda sana asije akanipoteza na mim nikamwambia hilo asiwe na shaka nalo
Ni mwanamke alieonekana yaan kama hela yangu haihitaji kabisa,hata nikimpa hela mfano 10,000 anasema acha tu nakuingiza kwenye matumizi ambayo ulikuwa hujayapangilia,basi kidume nikajiona nimepata mwanamke haswa yaan hana shida na hela yangu
Kumbe bhana alikuwa ananivuta mdogo mdogo,siku moja ananitumia sms nimuazimishe laki 1 baada ya wiki atanirudishia,nikatafakari sana ila nimeamua nimpe nione yatakayojiri,hata hivyo huwa napenda kuona na kuwasaidia wanawake wapambanaji,kwa kweli kwasasa nimeamini hawa wenzetu sio wa mchezo mchezo hawana time ya ujinga ni pesa tu.