Kuna Maadui wa aina 2, adui chanya na adui hasi

Kuna Maadui wa aina 2, adui chanya na adui hasi

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,380
Katika hii Dunia tunayoishi ambayo Wazungu wanasema ina Sayari takribani 9, wakati Mimi Deogratius Nalimi Kisandu najua fika Sayari iko moja tu ikiwa na Segment takribani 9 hivi.

Katika Dunia hii kuna umhimu sana wa kuwa na maadui kwani bila maadui huwezi kuwa imara na pia huwezi kuvumbua mambo ya kukukomboa wewe na Nchi yako. Kuna maadui wa ndani mwako na kuna maadui wa nje.

Kuna aina mbili kuu za maadui ambazo kila moja ina faida yake na hasara yake.

Aina ya kwanza ya Maadui ni:
POSITIVE ENEMY(Maadui Chanya).

Kundi hili la maadui wao lengo lao sio kukudhuru bali kukuona umekwama katika malengo yako na Mara nyingi huwa ni Wachawi ama wa mdomo au wakiimani. Hawa kazi yao nikukupa changamoto tu lakini hawana nia ya kutoa roho yako. Kupitia hawa unaimarika na kuwa Mtu mwingine ambaye unaweza kuwasababisha wao wakabadilika na kukusapoti. Hawa hata ukifanikiwa una haki ya kuwasaidia maana hawajui watendalo, na bado unaweza kufanya kazi nao vizuri tu. Pia kundi linaweza kuwa linatumika kwa maslahi ya watu wengine bila ridhaa yao.

Aina ya Pili ya Maadui ni:
NEGATIVE ENEMY(Maadui Hasi).

Kundi hili ni hatari sana na balaa, kazi yao wao ni kukuua kabisa katika malengo yako na kukuharibia, hawa wao ni wajinga na wapumbavu ambao uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. Hivyo wao kukuua ni sawa ili waonekane wao kuwa ni bora kuliko wewe. Kundi hili linaweza kufanya lolote mpaka ufe tu au upotee kabisa ili wao wafanikiwe kupitia mgongo wako. Kundi hili hata ukiwa mtawala sio kundi LA kushirikiana nalo kabisa. Ni kundi ambalo lazima ulipe kisasi na kuwasambaratisha kabisa maana wanaweza kufanya unyama ndani ya ushirikiano wao na wewe kama utawajali. Rejea vita vya wananchi kwa wananchi, rejea wagombea wa kisiasa na viongozi wa kisiasa.

Mimi nawatakia Siku njema na yenye mafanikio makuu.

Deogratius N Kisandu
3 January 2018.
 
yule nyoka aliekuingia katikati ya mapaja kwa nyuma alikuwa chanya au hasi?
 
Ila watu ni wabaya wanammega hadi chizi
 
Back
Top Bottom