Kuna maeneo ukikaa hapa Dar utaonekana ni wa hovyo

Ndio shida ya vijana kama ninyi mnaokuja kuishi Dsm kwa Shemeji. Ukifika Posta unaongea kwa kubonga ""oooh mimi nakaa posta - city center"".

Mpaka majina mnabadirisha mnajihita majina ya kishogashoga ""ooooh iam kimsboy""
Angalia kijana kunakuparamiwa.
 
Hayo ndio maeneo ya kuishi sasa, yaani heka heka za huko ni mguu wa shingo, mguu wa roho hakuna kupoa, hakuna kuboa mambo mpera mpera,

NB: Itoe Mbagala hapo ila kusema ukweli maeneo ya hivyo kwenye malezi ya watoto ni mtihani sana, wachache wamefanikiwa kimalezi.
 
Wewe una akili za enzi za Nyerere. Bado ushamba haujakutoka au uko Bariadi unasimuliwa tu kuhusu dar.
 
Wewe ni Fala Tu tena ni mshamba bado pia wewe ni wakuja hapa DAR.
Mimi nimezaliwa DAR nakushangaa Kwa kusifia UJINGA, hayo maisha tumeishi zamani miaka Ile ya 2002 tulikuwa tunasifia maeneo..

Nimesoma kinondoni na nimekulia kinondoni na sasa siwezi kuishi tena huko..wewe kiazi umeingia juzi mjini unaona imemaliza kilakitu kumbe bado mjinga
 
Utayaishi na ndiko unakoishi na hata kizazi chako watakuwa walala hoi daima
 
Mbagala Kuna mtu wangu wa maana Sana anaitwa David,Buguruni Kuna samweli,Kigogo Kuna Gody au muite G lover..vingunguti kwa kina Sadaat,Manzese ndio Kuna Wana kibao,mtoa mada wewe wa wapi??bila Shaka kutoka Nachingwea,city Boys wote tunajuana
 
Hahahaha
 
Wacha weee hata magomeni, duuh migo migo,magomeni mapipa lango la jiji

Sehemu nilizozitaja ni uswahilini hasa , huko ukae bachelor/single kama una familia hapafai kukaa utaharibu mke na watoto....Kino Ushuani ni pa kupahesabu labda Ada Estate ambayo ni kama mpakani na Oysterbay.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…