Uchaguzi 2020 Kuna mahali CCM ilikosea?

Uchaguzi 2020 Kuna mahali CCM ilikosea?

Nindi rais yupi aliruhusu magazeti ya Dar Leo na Alasiri. Awamu hii kimetokea nini
 
Wakuu heshima sana,

Kadri siku ya uchaguzi mkuu zinapokaribia nabaki najiuliza maswali kadhaa bila majibu.

Najaribu kutafakari ni eneo gani haswa CCM ilikosea ?.

Mosi,kununua wapinzani (wabunge,madiwani na viongozi wa vyama).Wananchi au ukipenda unaweza kuwaita wapiga kura hawapendi siasa za aina hiyo.
Ukinunua wabunge au madiwani yawezekana bado haujanunua wapiga kura au sababu za kuchagua upinzani bado zinakuwa pale pale !.

Pili,Style ya kutawala au kuongoza za utawala huu si rafiki au wapiga kura hawazipendi.Hivi siasa za kutumbua tumbua fukuza fukuza mara vyeti feki bado si jawabu la kupendwa ? !.Labda tuseme kulikuwa na uonevu,kukiuka sheria na taratibu za ajira au vyote kwa pamoja.

Tatu, Matumizi ya kupiliza ya vyombo vya habari kusifiwa na majivuno.TBC chini ya Dr Ryoba ilipitiliza kusifu kila jambo mara ndege,Reli,Vyeti feki lakini Makonda hausiki na ukaguzi.Barabara hata ya Kilometer 2 mtu atasifiwa kuanzia asubuhi hadi jioni kuanzia Jumatatu hadi Jumatatu nyingine ni mwendo wa kumsifu mtu mmoja ungefikiri kujenga Daraja au Kivuko ni hisani kumbe ni wajibu wake tena kazi yenyewe kaiomba kwa kampeni na ahadi luluki.

Nne,Unasema pekee yako miaka mitano wengine wakisema shida (Kesi,Vifungo,misukosuko....)Nauliza WaTanzania wamechoka na siasa za aina hii !.

Tano,Ujenzi wa Flyover Dar una faida zipi kwa mkaazi wa Dongobesh au Tarakea mkulima wa ndizi au mkulima wa Ngogwe Lushoto.Naamini kila eneo la nchi yetu lina mahitaji yake ya msingi kutokana na mazingira yake.

Sita,Watawala wetu walifika mahali wakajiona hapo walipo walifika wenyewe si wananchi /wapiga kura.Kauli zao maamuzi yao mengi yalilenga kuwanufaisha wao wenyewe eg kupitisha sheria za kuwajengea nyumba MaRais wastaafu,Sheria za mafao yao na matibabu yao zipo vizuri kweli kweli wakati wafanyakazi sheria za mafao yao kila mara wanatengenezewa sheria za kuwakandamiza eg sheria ya kujitoa na kikokoteo.Sheria za kinga ya kutoshitakiwa hata wakifanya makosa ya aina gani !.

Mwisho nadhani watawala hawakujiandaa kukumbana na uchaguzi wenye ushindani wa kiwango hiki tunachokiona sasa.Walifikiri kumnunua Silinde,Lijualikali,Nassari ...... watakuwa wamemaliza kila kitu sasa wamekutana na uungwaji mkono wa kiwango cha kutisha kutoka kwa mgombea wa CHADEMA.
Tangu mfumo wa siasa wa vyama vingi kuanzishwa tumewaona wagombea walioleta kashi kashi za kutisha.Mwaka huu 2020 tumeanza kuona dalili mbaya kwa baadhi ya mikoa ambayo chaguzi za nyuma walikuwa wakiunga mkono CCM.Mkoa ya Rukwa,Sumbawanga,Katavi,Simiyu,Ruvuma,Lindi na Mtwara ni ngome ya CCM kwa muda mrefu lakini tumeshuhudia katika uchaguzi huu wananchi wa mikoa hiyo wakibadilika na hivyo kuiweka CCM katika wakati mgumu.
Kunyima watu haki ya kuishi uhuru wa kuwaza tofauti, kukusanyika, kufanya mambo yao bila uoga na hofu watakupinga tu.
 
Kaka ilosioswali kaka angalia kwa wavuvi tu unakutwa na chombo chako kinataratibu zote zinazotakiwa alafu mtu kwa tamaa zake nakujidaia madaraka anasema leteni pesa kama hamna pesa nazichoma mm nimetumwa pesa nimeambiwa kama huna pesa nichome
Naapa nilipo simsikilizi yoyote awe mkuu wawilaya au mkuu wamkoa ninawasikiliza waziri na rais tu ndiowalionituma onajamaa alivyo tufilisi kwa tamaa ilitumuabudu mungu atamuonyesha roho inaumasana
 
IMG_20201018_181535.jpg
 
Ilikosea kila kona, hasa Kawe kumteua Gwajima
Kupitisha sheria kandamizi kwa wananchi kama sheria ya vyombo vya habari, sheria ya takwimu na sheria ya vyamana vya siasa huku wao wakikazana kujiwekea kinga.

Sasa kama unafanya kitu sahihi na unajiamini Kuna haja gani ya kupambana kujiwekea kinga ili wasiwajibishwe?
Huku ni kujifanya miungu watu na TUNAKATAA.
 
Kiongozi yeyote anayejifanya Mungu ni lazima aanguke , Magufuli aliwaambia wajumbe wa Kamati kuu ya ccm kwenye kikao kilichofanyika ikulu kwamba " Waacheni waliolemewa na mizigo waje kwangu nami nitawapumuzisha " hapa alizungumzia wale wabunge na madiwani waliojiuza kwa bei rahisi na kuhamia ccm , kauli hii ilikuwa ya kujitafutia laana kutoka kwa Mungu .

Watu wote wenye akili timamu walijitenga na awamu hii , wengi waliobaki walikuwa wenye madaraka na wachumia tumbo , baada ya kugundua kwamba wenye akili wamejitenga ndio ukaasisiwa mtindo mpya wa kishamba wa Kudukua simu za watu ili kujua wanachoongea baada ya kujitenga .

Kwa ujumla mbinu mbovu za viongozi duni wa ccm makao makuu wakiwemo Bashiru na Polepole kumeangamiza ccm , viongozi hawa kwa bahati mbaya sana waliamini wana akili kuliko Watanzania wote nchi nzima , kitu ambacho ni kichaa pekee anayeweza kufikiri hivyo
 
Unasikia mtawala anasema mimi sipangiwi !.
Sasa hivi anapiga magoti 😂 😂 😂 watanzania sio watu wazuri

Yule baba jinsi anavyopenda visasi kwakuwa watanzania mmempigisha magoti akirudi ikulu laza awarushe watanzania wote vichura chura ....tujiandae tu kisaikolojia 😂 😂
 
Kutegemea dola badala ya hoja, wameitumia police kuuwa upinzani imeback fire polisi wamechangia kuimarika kwa upinzani Hadi vijijini.
Lolote baya walilowatendea watz limerudi kwao mara 7.
.wamebandika mabango nchi nzima.
.wamezuia media zote
.wametumia wasanii wote
. wanatumia police
. wametumia time
.wametumia msajili
Lkn vyoote vimebuma.
Chama mfu Ni kile kinachobebwa na dola badala ya nguvu ya umma. Anaemiliki nguvu ya umma ndie anaemiliki dola.
Yaani kama hii issue ya kuzuia mabango daahhh !!!! Inadhihirisha kabisa kuwa jamaa wanaroho za kichawi ma hawana nia njema na Watanzania ...haiwezekani raia wa nchi 1 wengine wakawa wanawabagua wenzao na kuwatesa kiasi hiki .....siku ccm ikiondoka madarakani nitatembea kwa miguu dar mpaka moro kwaajili ya furaha mitakayo kuwa nayo
 
Ngongo kuna 'mahali' gani CHADEMA yako ilipatia?

Kwanza CHADEMA haijawahi kuwa yangu labda itakuwa yangu sasa kwasababu inahubiri habari ya haki,uhuru na maendeleo.

CHADEMA mwaka 2015 ilikosea kumsimamisha mgombea aliyeshindwa kutetea ilani ya chama chake.Mbaya zaidi alijiunga CHADEMA kwakuwa alipewa nafasi ya kugombea uRais.

Uchaguzi huu 2020 mgombea ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kufafanua mambo mbali mbali ambayo mgombea wa CCM kakosea eg ujenzi wa Chato International Airport,Fao la kujitoa,Uhuru wa kukutana na kutoa mawazo mbadala,Undugunization katika teuzi mbali mbali eg Katibu Mkuu Hazina.
 
'Mnafiki' huwa 'hajifichi' halafu ni mwepesi sana Kugundulika / Kujulikana.
 
Back
Top Bottom