Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Tunaweza kuwalaumu, tunaweza kuwabebesha kila aina ya lawama na pia tunaweza kuwabeza, kuwakejeli, na kuwanyoshea vidole. Ukweli utabakia kuwa yawezekana siyo kosa lao peke yao; ni kosa letu pia.
Kuna mahali tulipopotea njia, au mahali ambapo tulikwepa kufanya tulichotakiwa kufanya na matokeo yake tupo hapa tunarushiana maneno, madongo na kila aina ya lawama. Yawezekana ni rahisi kumtaja mtu mmoja na kusema huyu ndiye anawajibika kwa kupotea njia, au kutaja kikundi kimoja cha watu na kusema "wale" ndio wanawajibika kwa sisi kujikuta hapa tulipo.
Hata hivyo yawezekana kabisa kuwa mzigo huu wa lawama unatakiwa kubebwa na watu wengi kama siyo Taifa zima. Kuna kitu hatukifanya tulipotakiwa kufanya na hivyo leo hii tunalipia gharama yake.
Kuna kitu ambacho nchi tulizokuwa nazo sawa na ambazo bado zina mambo mengi ya kuwakera zimekuwa zikifanya vizuri na kuanza kufuata njia sahihi. Iran, Indonesia, Malaysia, South Korea, India, na sasa Liberia, Rwanda, Congo, Angola na South Afrika..
Je yawazekana mgongano utakaotokea mwishoni mwa juma (ceteris paribus) utakuwa ni chachu ambayo itaturudisha kwenye njia sahihi kuelekea kule tunakotaka kwenda?