Kuna maisha baada ya uchaguzi

Kuna maisha baada ya uchaguzi

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (55)✍️
Waswahili husema; "Mungu hakupi vyote na wala hakunyimi vyote". Hivyo sina budi kusema watanzania hawakunyimwa amani, upendo, na utulivu. Mwaka 2024 & 2025 watanzania wanatarajia kufanya uchaguzi mdogo na uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wao wa kisiasa.

Ni kipindi ambacho watanzania watapitia nyakati tatu (3) ambazo ni; wakati wa kampeni, wakati wa kupiga kura, na wakati wa kutangaza matokeo. Hivyo katika nyakati zote tatu watanzania hawapaswi kusahau kuwa hawakunyimwa amani, upendo, na utulivu. Kwa hiyo wasipoteze hicho walichopewa.

Kipindi hiki cha uchaguzi ewe Mtanzania unapaswa kukumbuka kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi. Kamwe usianzishe....
❌Vita ya matusi,
❌Vita ya ugomvi,
❌Vita ya kudhuru mwili, akili, au hisia,
❌Vita ya kulipa kisasi,
❌Vita ya kuua mtu.....

Au vita mbaya yoyote kwa Mtanzania mwenzako kwasababu ya upepo wa kisiasa. Huu ni upepo ambao unapita kisha unakuacha wewe ukiendelea kuishi na watu wanaokuzunguka. Kuna maisha baada ya uchaguzi.

Huwezi kuishi mwenyewe bila kumtegemea mtu mwingine hata kama una pesa nyingi. Hujui kesho Mungu atakupeleka kwa nani ili ukaombe msaada wa kumponya mwanao, mzazi, au ndugu yako au wewe mwenyewe. Hivyo usianzishe vita na mtanzania mwenzako.

✓ Tambua kuwa unaweza kuanzisha vita na mtu ambaye ameandaliwa na Mungu kwa ajili ya kukupeleka hospitali pindi ukiwa hujiwezi kitandani kwako.

✓ Tambua kuwa unaweza kuanzisha vita na mtu ambaye ameandaliwa na Mungu kukusaidia wewe, au kuwasaidia ndugu zako katika pilika za mazishi ya mtoto, ndugu, au mzazi wako.

✓ Tambua kuwa unaweza kuanzisha vita na mtu ambaye ameandaliwa na Mungu kukubeba pindi ukiwa umeanguka barabarani na hujitambui.

✓ Tambua kuwa unaweza kuanzisha vita na mtu ambaye ameandaliwa na Mungu kukata mkanda wa siti ya gari (seat belt) ambao utakubana wakati utakapopata ajali - ili kukuepusha na kifo cha mlipuko wa moto.

✓ Tambua kuwa unaweza kuanzisha vita na wateja wako muhimu sana ambao hawakosi kukuungisha kwenye biashara yako. Na baada ya uchaguzi kupita utawasubiri wakuungishe.

✍️What goes around, comes around. Hivyo hupaswi kusahau kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi mdogo (2024) na uchaguzi mkuu (2025).

Right Marker
Dar es salaam.
 
Sijui kama watakuelewa.
 
Back
Top Bottom