Kuna Majamaa wanaambukiza mabinti HIV makusudi

ZITTO ameshawaaribu na huu msemo wa ""majina ninayo, na ushahidi ni nao""
 
ila so long as they fall to him diplomatically and wameshafika umri wa ki utu uzima kisheria jamaa hana makosa .....

Kama ndio hivyo basi sheria zetu zina mapungufu makubwa sana!!! Kuambukiza mabinti sio kosa kumbe endapo hao mabinti wapo >18+
 
Ni mamlaka ipi huitaji USHAHIDI, Mahakama au Wapelelezi(Polisi)?
Ni mamlaka ipi inahitaji vidhibiti, Mahakama au Wapelelezi(Polisi)?

Right. Kumwambukisa mtu Ukimwi kwa kusudia au kwa makusudi ni kosa la jinai.

Kwa hiyo, kama umeona au una-suspect kuwa kuna mtu anaambukiza ukimwi kwa njia hizo then unaweza kum-ripoti polisi ili wafanye uchunguzi wao.

Watachunguza vipi, wanajua wenyewe, lakini utakuwa unawasaidia kwenye uchunguzi wao. Kama ikidhibitika kuwa mhusika siyo tuu ana ukimwi bali pia ameshawaambukiza watu, then anaweza kufikishwa mahakamani.

Akishafikishwa mahakamani, kuna uwezekano mkubwa wewe ukawa mmoja wa mashahidi. Pia hao walioambukizwa itabidi watokee mahakamani kama mashahidi.

Lakini vipi mhusika akidai kuwa wakati anafanya nao mapenzi hakujua kama ana Ukimwi? Wewe umejuaje?
 
ZITTO ameshawaaribu na huu msemo wa ""majina ninayo, na ushahidi ni nao""

Ndio maana nimesema kama kuna taasisi ipo niwape namba za simu na location za hao watu wawekee mitego wawatie hatiani lkn swali,je sheria zetu zinasemaje? Unaweza ukawakamata lkn wakashinda kesi ukawa umepoteza mda wa bure tu!! Maana bila kufanya hivi maambukizo hayawezi kwisha.
 
Kwani UKIMWI ni ugonjwa wa kuambukizana? hakunaga kitu hicho na hiyo HIV aliigunduwa nani vile?, mkuu pamoja na uelewa wetu mdogo kuhusu UKIMWI bado hao jamaa hawawabaki, wanawatongoza na hela wanawapa, waache watumie pesa yao.

Mkuu jiheshimu kidogo. Hivi wangekua ni dada zako wanafanyiwa hivyo ungeandika huu utumbo humu?
 

EMT ndio maana nimelileta huku tuliangalie kisheria zaidi ili tukiamua kuwapeleka front tushinde kesi na watiwe hatiani,kwa miwaya 100% ni hiv+ ila wanavyofanya hyo tabia ya ngoja na mimi niambukize wengine ndio balaa!
 
Last edited by a moderator:

Naomba niulize, sheria za Tanzania zilipitisha lini kuwa kumuambukiza mtu VVU kwa kukusudia ni kosa la jinai?

Naomba kifungu cha sheria kama unacho kwa future reference
 

Hili swali jibu lake nadhani si gumu sana, maana kwa sheria zetu ili ufikishwe mahakamani angalau lazima kuwe na ushahidi wa kuanzia au vidhibiti vinavyokuhusisha moja kwa moja na kosa. Ushahidi huu hufanywa na Polisi au Mamlaka zenye kuruhusiwa kikatiba kulingana na muktadha wa kosa bainifu.
Sasa basi kwa kuwa mleta anahisi kuna walakini katika afya za hao rafikize, ndio maana kaleta bandiko lake ili kufahamishwa kama kuna mamlaka au chombo ambacho kinaweza kufanya uchunguzi ili hao rafikize wasiendelee kufanya maambukizi zaidi.
Maana yangu ya kuibua mjadala, ni hoja aliyoiweka yule jamaa aliyekua anauliza "una ushahidi?"...maana ukishaanza kuibua swali kama hilo ina maana wananchi wasipeleke TUHUMA kwenye Mamlaka husika
 

Ukiachana na sheria ya makosa ya jinai, sheria husika ni The HIV and AIDS (Prevention and Control) Act 2008. Chini ya kifungu cha 4, wewe kama King Kong III na mimi kama EMT tuna general obligation ya kuzuia kunea kwa ukimwi. Kwa hiyo kama kuwaripoti watu ambao unadhani wanaambukiza ukimwi kwa kukusudia, kwa makusudi au hata kwa kutokusudia utakuwa umeplay part yako ya kupunguza kuenea kwa Ukiwmi. Naweza kusema siyo legal obligation tuu bali pia ni moral obligation.

Kifungu cha 47 cha sheria hiyo kinasema kuwa mtu ambaye anasambaza Ukimwi kwa kukusudia atakuwa ametenda kosa na akishtakiwa anaweza kufungwa kati ya miaka mitano na kumi. Pia kifungu cha 48 kinasema kuwa mtu mbaye kwa kukusudia hafuati safe procedures and practices na kusababisha kuenea kwa Ukimwi atakuwa pia ametenda kosa.

Mwisho kifungu cha 51 kinaeleza jinsi ya kulalamika kama unaona kuna mtu yoyote anayeenda kinyume na hii sheria. Unaweza kutuma malalamiko yako kwa maandishi kwenda kwa wafuatao:


  1. katibu wa kijiji, kata, wilaya au urban AIDS commitees
  2. Police station
  3. Mwajiri (wa unayemshuku nadhani)
  4. Mmiliki au incharge wa health centre (kama haitumii safe procedures and practices)

Malalamiko yote lazima yatoe maelezo muhumu kuhusiana na lalamiko lenyewe. Pia Waziri husika anaweza akaongeza njia nyingine ya kutuma malalamiko (sijui kama kuna njia nyingine iliyowekwa na waziri).
 
Naomba niulize, sheria za Tanzania zilipitisha lini kuwa kumuambukiza mtu VVU kwa kukusudia ni kosa la jinai?

Naomba kifungu cha sheria kama unacho kwa future reference

Cheki post namba 30 hapo juu in relation to spreading HIV.

Lakini pia zipo general laws kuhusiana na grievously bodily harm.
 

Ngoja nianze na kijiji+Polisi ila itabidi nitume as Anon maana hawa polisi na watu wa serikali hawakawii kusema king ndio kaleta hii barua hapa!!
 
Cheki post namba 30 hapo juu in relation to spreading HIV.

Asante sana

Jee sheria hiyo inamuangaliaje daktari?

Kwa mfano daktari anajua Bwana A ana VVU, kwa sababu yeye ndio aliyempima na anajua anachukua ARV kwa miaka mingi. Akatokea mkewe Bwana A akaumwa UKIMWI ila mkewe akasema hajui lolote kuhusu status ya mumewe na wala hawakuwa wakifuata procedures zozote za kujikinga.

hapa daktari anatakiwa kuchukua hatua gani?
 

Personally, sipendi the so called "ushahidi wa kuanzia". Hiyo ndiyo inayosababisha kesi nyingi zinakuwa delayed na watu kusekwa ndani ovyo, kisa eti "uchunguzi bado unaendelea". Worse hata uchunguzi ukikamilika unakuta ushahidi is so weak na kuamua ku-drop kesi, ambayo imekuwa ikitajwa kwa miaka mpaka mpaka mitatu huku mtuhumikwa akiwa ndani.

Bora mtu afikishwe mahakamani na kushtakiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi na kupatatikana kwa ushahidi wa kutosha. Tatizo la polisi wetu wakiletwa allegation, wanachofanya kwanza ni kwenda kumkamata mtuhumiwa na kuanza kufanya uchunguzi. Matokea yake unampa mtuhumiwa nafasi ya kuharibu ushahidi wote.

Unamkumbuka jinsi polisi wa Uingereza walivyomfuatilia yule Mtanzania aliyekamatwa na kushtakiwa nchini Uingezereza kwa kuiba posh cars na kuyaleta Tanzania? https://www.jamiiforums.com/habari-...uk-police-nailed-dar-young-millionaire-3.html

Umshaangalia movie kama Goodfellas, American Gangster, n.k. jinsi wanavyokusanya ushahidi huku wakiwaacha watuhumiwa wakifanya kama wapendavyo lakini wakishaamua kuwakama ni moja kwa moja mahakamani. Jamaa wakionyeshwa ushahidi wenyewe wanakubali.
 
Ngoja nianze na kijiji+Polisi ila itabidi nitume as Anon maana hawa polisi na watu wa serikali hawakawii kusema king ndio kaleta hii barua hapa!!

Unabidi ucheki nao kabla, maana kuna organisations nyingine hazi-deal na Anonymous complaints.

Some might regard them as frivolous complaints or complaints filed with ill-will or malice. Wengine watakaka kuku-verify kama mlalamikaji and pia kuangalia credibility ya facts and evidence.

Pia kama complaint ni serious, watashindwa kukupata kwa information zaidi, uless uwe umeelezea kila information inayohitajika kwenye hiyo complaint.

Tatizo tulilonalo Tanzania ni kwamba ukitoa lalamiko lazima utajulikana tuu. Tunapenda sana habari za udaku.
 

Anaitwa Mponjoli Malakasuka kama sijakosea....

Hizo movies nimeshaziona mkuu na unachokisema ni kweli kabisa, lakini ni vyema tukatazama upya muundo wa USHAHIDI, MTUHUMIWA, MSTAKIWA katika huu mchakato mpya wa katiba...
 
You have to prove beyond the reasonable doubt before the court of law, do you have an HIV/AIDS medical examined report of those two suspects from medical expert, so that to stand as evidence? If not your charge will be dismised
 
Ngoja nianze na kijiji+Polisi ila itabidi nitume as Anon maana hawa polisi na watu wa serikali hawakawii kusema king ndio kaleta hii barua hapa!!

mbona kama una uoga! Ukiamua kulivalia njuga swala inabidi uwe tayari kwa lolote. Shukrani kwa EMT.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: EMT

Nafikiri daktari anaingia kwenye hicho kifungu cha 4 maana kinasema kina-impose hiyo "general obligation" to "every person". Lakini kama daktari ana duty of confidentiality (kifungu cha 17), tuliyoijadili kwenye ile thread ya technician kusambaza habari za aliowapima na kuwakuta wakiwa na Ukimwi.

Hata hivyo, kifungu cha 16(2) kinasema kuwa test results, though confidential, may be released to, among others, "a spouse or a sexual partner of an HIV tested person".

Sasa kama daktari alikuwa anajua A ana Ukimwi na ana mke, alikuwa na "general obligation" kwa mujibu wa kifungu chan 4, kumfahamisha mkewe. Hii ingesaidia, kwa mujibu wa kifungu cha 4, ku-prevent HIV (kama huyo mke alikuwa bado hajaambukizwa) au ku--control (kama alikuwa tayari ameshaambukizwa).

Pia angeweze ku-release testing results kwa mke wa Bwana A kwa mujibu wa kifungu cha 16(2). Kama huyu Bwana A angekuwa anaishi kwenye nchi zilizoendelea, baada ya daktari kumpima na kumkuta na Ukimwi, lazima angempima pia mkewe.

Having said that, hii ni tafsiri yangu binafsi. Daktari yoyote Tanzania anatakiwa atafute kwanza a proper legal advise kabla ya ku-revel confidential information hasa za watu ambao wamewapima na kuwakuta wana Ukimwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…