Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ila so long as they fall to him diplomatically and wameshafika umri wa ki utu uzima kisheria jamaa hana makosa .....
Ni mamlaka ipi huitaji USHAHIDI, Mahakama au Wapelelezi(Polisi)?
Ni mamlaka ipi inahitaji vidhibiti, Mahakama au Wapelelezi(Polisi)?
ZITTO ameshawaaribu na huu msemo wa ""majina ninayo, na ushahidi ni nao""
Kwani UKIMWI ni ugonjwa wa kuambukizana? hakunaga kitu hicho na hiyo HIV aliigunduwa nani vile?, mkuu pamoja na uelewa wetu mdogo kuhusu UKIMWI bado hao jamaa hawawabaki, wanawatongoza na hela wanawapa, waache watumie pesa yao.
Right. Kumwambukisa mtu Ukimwi kwa kusudia au kwa makusudi ni kosa la jinai.
Kwa hiyo, kama umeona au una-suspect kuwa kuna mtu anaambukiza ukimwi kwa njia hizo then unaweza kum-ripoti polisi ili wafanye uchunguzi wao.
Watachunguza vipi, wanajua wenyewe, lakini utakuwa unawasaidia kwenye uchunguzi wao. Kama ikidhibitika kuwa mhusika siyo tuu ana ukimwi bali pia ameshawaambukiza watu, then anaweza kufikishwa mahakamani.
Akishafikishwa mahakamani, kuna uwezekano mkubwa wewe ukawa mmoja wa mashahidi. Pia hao walioambukizwa itabidi watokee mahakamani kama mashahidi.
Lakini vipi mhusika akidai kuwa wakati anafanya nao mapenzi hakujua kama ana Ukimwi? Wewe umejuaje?

Ndio maana nimesema kama kuna taasisi ipo niwape namba za simu na location za hao watu wawekee mitego wawatie hatiani lkn swali,je sheria zetu zinasemaje? Unaweza ukawakamata lkn wakashinda kesi ukawa umepoteza mda wa bure tu!! Maana bila kufanya hivi maambukizo hayawezi kwisha.
Naomba niulize, sheria za Tanzania zilipitisha lini kuwa kumuambukiza mtu VVU kwa kukusudia ni kosa la jinai?
Naomba kifungu cha sheria kama unacho kwa future reference
Ukiachana na sheria ya makosa ya jinai, sheria husika ni The HIV and AIDS (Prevention and Control) Act 2008. Chini ya kifungu cha 4, wewe kama King Kong III na mimi kama EMT tuna general obligation ya kuzuia kunea kwa ukimwi. Kwa hiyo kama kuwaripoti watu ambao unadhani wanaambukiza ukimwi kwa kukusudia, kwa makusudi au hata kwa kutokusudia utakuwa umeplay part yako ya kupunguza kuenea kwa Ukiwmi. Naweza kusema siyo legal obligation tuu bali pia ni moral obligation.
Kifungu cha 47 cha sheria hiyo kinasema kuwa mtu ambaye anasambaza Ukimwi kwa kukusudia atakuwa ametenda kosa na akishtakiwa anaweza kufungwa kati ya miaka mitano na kumi. Pia kifungu cha 48 kinasema kuwa mtu mbaye kwa kukusudia hafuati safe procedures and practices na kusababisha kuenea kwa Ukimwi atakuwa pia ametenda kosa.
Mwisho kifungu cha 51 kinaeleza jinsi ya kulalamika kama unaona kuna mtu yoyote anayeenda kinyume na hii sheria. Unaweza kutuma malalamiko yako kwa maandishi kwenda kwa wafuatao:
- katibu wa kijiji, kata, wilaya au urban AIDS commitees
- Police station
- Mwajiri (wa unayemshuku nadhani)
- Mmiliki au incharge wa health centre (kama haitumii safe procedures and practices)
Malalamiko yote lazima yatoe maelezo muhumu kuhusiana na lalamiko lenyewe. Pia Waziri husika anaweza akaongeza njia nyingine ya kutuma malalamiko (sijui kama kuna njia nyingine iliyowekwa na waziri).
You have some screws missing upstairs, I bet
Cheki post namba 30 hapo juu in relation to spreading HIV.
Hili swali jibu lake nadhani si gumu sana, maana kwa sheria zetu ili ufikishwe mahakamani angalau lazima kuwe na ushahidi wa kuanzia au vidhibiti vinavyokuhusisha moja kwa moja na kosa. Ushahidi huu hufanywa na Polisi au Mamlaka zenye kuruhusiwa kikatiba kulingana na muktadha wa kosa bainifu.
Sasa basi kwa kuwa mleta anahisi kuna walakini katika afya za hao rafikize, ndio maana kaleta bandiko lake ili kufahamishwa kama kuna mamlaka au chombo ambacho kinaweza kufanya uchunguzi ili hao rafikize wasiendelee kufanya maambukizi zaidi.
Maana yangu ya kuibua mjadala, ni hoja aliyoiweka yule jamaa aliyekua anauliza "una ushahidi?"...maana ukishaanza kuibua swali kama hilo ina maana wananchi wasipeleke TUHUMA kwenye Mamlaka husika
Ngoja nianze na kijiji+Polisi ila itabidi nitume as Anon maana hawa polisi na watu wa serikali hawakawii kusema king ndio kaleta hii barua hapa!!
Unamkumbuka jinsi polisi wa Uingereza walivyomfuatilia yule Mtanzania aliyekamatwa na kushtakiwa nchini Uingezereza kwa kuiba posh cars na kuyaleta Tanzania? https://www.jamiiforums.com/habari-...uk-police-nailed-dar-young-millionaire-3.html
Umshaangalia movie kama Goodfellas, American Gangster, n.k. jinsi wanavyokusanya ushahidi huku wakiwaacha watuhumiwa wakifanya kama wapendavyo lakini wakishaamua kuwakama ni moja kwa moja mahakamani. Jamaa wakionyeshwa ushahidi wenyewe wanakubali.
Ngoja nianze na kijiji+Polisi ila itabidi nitume as Anon maana hawa polisi na watu wa serikali hawakawii kusema king ndio kaleta hii barua hapa!!
Asante sana
Jee sheria hiyo inamuangaliaje daktari?
Kwa mfano daktari anajua Bwana A ana VVU, kwa sababu yeye ndio aliyempima na anajua anachukua ARV kwa miaka mingi. Akatokea mkewe Bwana A akaumwa UKIMWI ila mkewe akasema hajui lolote kuhusu status ya mumewe na wala hawakuwa wakifuata procedures zozote za kujikinga.
hapa daktari anatakiwa kuchukua hatua gani?