mchawi wa kusini
JF-Expert Member
- Apr 18, 2018
- 830
- 898
Kabila la Hamer na desturi ngumu
Kabila la hamer linalopatikana kusini mwa nchi ya Ethiopia ndilo kabila linalosifika kudumisha mila na desturi ya kuthibitisha uwezo wa mwanamke kuvumilia magumu kwenye ndoa!
Inasemekana mwanaume kabla hajatoa mahari inabidi ampime mwanamke anayetaka kumuoa kama atakuwa na uvumilivu wa shida na raha katika ndoa! Kipimo hicho ni kwamba mwanamke anatakiwa mwenyewe atafute fimbo nzuri na kumkabidhi mwanaume, na hapo mwanaume anatakiwa amcharaze fimbo za kutosha mwanamke huyo na hatotakiwa kuonyesha ishara yeyote ya maumivu wala kulia na akifanikiwa kwa hilo basi mwanamke huyo atakuwa na sifa ya uvumilivu na mahari kubwa itatolewa kwake!
Ninachoshindwa kuelewa ni namna ambavyo wasichana hao wanaweza kuvumilia hali hio ngumu,fimbo ya kupasua kabisa na kuharibu ngozi,kisa ndoa!Ndiyo ni mila,lakini huu kwangu mimi naona ni ukatili mkubwa kwa wanawake hawa!Hata ingawa inasemekana hawa ndoa zao hazivunjikagi,wanaishi sana kwenye ndoa....ila....mmh!
Nini maoni yako!