Kuna Makosa kwenye chaneli ya WhatsApp ya Rais Mwinyi

Kuna Makosa kwenye chaneli ya WhatsApp ya Rais Mwinyi

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
345
Reaction score
307
Nimekuwa mfuatiliaji wa taarifa za viongozi wanazoweka katika kurasa zao binafsi za kwenye Chanel za WhatsApp.

Hizi kurasa ni mbali na zile zinazotangaza kazi rasmi za ofisi zao.

Naomba nitoe mfano wa kurasa hizo na baadhi ya viongozi kabla sijaeleza Makosa ninayokusudia yarekebishwe.

Kwenye ukurasa wa Chanel ya WhatsApp ya Rais Samia ukiingia utaona anayezungumza ni yeye mwenyewe akieleza kile anachokusudia,vile vile ukurasa wa Zitto Kabwe,January Makamba na hata Dorothy Semu ambaye ni kiongozi wa ACT Wazalendo.

Ukienda katika ukurasa binafsi wa Rais Mwinyi,humuoni akizungumzia kile alichofanya bali na yeye ni kama anamtolea taarifa mtu mwingine.

Mfano badala ya kusema "Leo nimefanya uteuzi" unakutana na neno Rais Mwinyi afanya uteuzi au Rais Mwinyi afanya hili na lile.

Kiuhalisia hiyo inaharibu maana nzima ya kuwa na Chanel binafsi kwa maoni yangu.
 
Kwahiyo unaamini hiyo account ya Samia anaiendesha yeye mwenyewe? Alafu kumfananisha Mwinyi na vitu vya ajabu ( Zito)
 
Back
Top Bottom