Gobole Lenye Risasi
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,519
- 23,693
Alizuia Uholela. Uholela wa wafanyabiashara kujiuzia watakavyo baadhi ya vitu. Na ulanguzi. Alifanikiwa kwa kiasi flani. Nakumbuka zamani hata Fuel ambayo walikuwa wakiuza TOTAL ilikuwa bei ya juu kidogo ukilinganisha na wadau wengine.
Total walikuwa wao hawafuati bei Elekezi. Walikuwa na bei yao wao ya juu kidogo. Alikuja waweka sawa. Wakawa nao wanafuata bei elekezi kama wadau wengine.
Leo hali imebadilika. Mwanza kuna vituo vya mafuta vinauza petrol tsh 3400+ vipo. Na havina wasiwasi kabisa sababu vinajua sababu ya wao kuuza bei hiyo. Siwalaumu wahusika.
Nauli za Mabus pia bei elekezi imeachwa wameongeza zaidi mpaka 5000 kutoka kwenye bei elekezi.
Sasa mtatusamehe sisi tunaolalamika ni maskini na hatuwezi miliki magari maana ndo excuse kuwa kama huwezi kununua mafuta kwa bei ya juu basi hukufaa kumiliki gari. Ninyi matajiri sasa kwa nini badala ya tsh 3100+ msinunue kwa 5000 ili kuwafidia hawa maskini ambao sasa kila kitu itasingiziwa vita ya Ukraine na Russia?
Tufike wakati tujiheshimishe. Tunayofanya sasa michezo yenu mauti yetu ila ipo siku watu watachoka kwa huu uonevu na unyanyasaji kwa wananchi. Wananchi wamekuwa ni kama hawana Baba wala Mama.
Magufuli hakuwa malaika. Alikuwa na mapungufu yake na tulikuwa tunapingana kwenye baadhi ya mambo. Na tuna kubaliana kwenye baadhi ya mambo. Wanasiasa Wafanyabiashara wameshika Hatamu.
Kuna viongozi watatu. Wanaagiza mafuta kwa sasa mmoja ni mstahafu na wawili wapo kwenye Serikali hii na Chama. Hawa ndiyo wanaoratibu kwa kiasi kikubwa hizi bei na wakisema kuwa wanapaswa kufidia hasara ambazo waliingizwa.
Lakini pia kutengeneza pesa kwa ajili ya chaguzi zijazo kama ambavyo wanamwaminisha yeye. Kuwa awaache wafanye biashara kukusanya pesa za kampeni maana kuna ukinzani dhidi yake. Naye ameamini hilo.