Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Huko nchini Kenya, uteuzi wa mawaziri unachukua mchakato mrefu, Hadi Waziri huyo aapishwe.
Hatua anazopitia Waziri huyo baada ya kupendekezwa na Rais kuwa Waziri ni jina lake kupelekwa Bungeni, Ili apitie katika "chekecho" ikiwa nafasi hiyo anastahili na iwapo wabunge hao wataridhika kutokana na maelezo ya Mbunge huyo mteule, ndipo jina Hilo linarudi Ikulu Ili aapishwe rasmi.
Kwa mfano katika hili sakata la vijana wa Gen Z wa Kenya walivyofanya maandamano nchi nzima, kushinikiza Baraza Zima la mawaziri watimuliwe, ndipo Rais Ruto, akatii amri hiyo na kupendekeza Baraza lingine la mawaziri 20 na kuyapeleka Bungeni, ambapo baada ya hao mawaziri waliopendekezwa na Rais Ruto kuhojiwa na Bunge Hilo, Waziri mmoja, hakupitishwa katika "kiti moto" hicho Cha wabunge.
Ndipo hivi leo nimeshuhudia Rais Ruto akiwaapisha mawaziri hao 19, bila jina la huyo Waziri wa jinsia Stella Soy, ambaye hakupitishwa Bungeni
Mambo ni tofauti kabisa hapa nchini kwetu, ambapo Rais akikuteua ndiyo Moja Kwa Moja "umeula" unasubiri kuapishwa na kuwa Waziri!
Ndiyo maana katika nchi yetu, machawa Kwa Rais Samia, wamekuwa wengi mno, Kwa kuwa wanamchukulia Rais wetu kama mungu-mtu, lile alifanyalo halipaswi kusahihishwa na Binadamu mwingine yoyote yule.
Hivi kweli tunategemea kupata maendeleo katika nchi hii, iwapo hata huo uteuzi utakuwa unaofanyika "kishikaji" ambapo hata kama wananchi tutakuwa tunajua kuwa aliyeteuliwa ana historiia ya maovu mengi sana aliyoyatenfa kabla, hakuna nafasi ya kupinga!
Kwa maana hiyo zipo sababu za msingi kabisa, zinazotolewa na mamilioni ya watanzania, kuwa ni LAZIMA tuwe na Katiba mpya ya nchi, ambayo itaondoa huo mfumo wa kumgeuza Rais wetu kuwa mungu-mtu itakayolingana na mazingira ya sasa ya nchi yetu
Mungu ibariki Tanzania