Kuna mashirika yako vizuri mpaka raha yani

Kuna mashirika yako vizuri mpaka raha yani

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Kuna NGO nilifanya nao first interview last week kwa njia ya zoom meeting,sasa juzi wakanipigia kuwa leo niende kwa second interview pale ofisini kwao mikocheni.

Tulikua mtu kama 8 au 7 hivi kama sikosei.tumepiga interview mpaka saa 7 mchana,sasa kila msailiwa alikua akitoka kwenye chumba cha usaili anapewa 50,000/=wanakuambia it is for transport cost+lunch.

Aisee wale jamaa atakaebahatika kupata hiyo kazi atakua kasahau shida za ulimwengu kwa muda.kwanza wenyewe hawana cha kuficha kuhusu mambo ya salary,pale pale kwenye interview wametuambia our budget for this position is 2,857,000/= PM.

Kwa kweli nimewapenda bure.

Haka ka 50k walikonipa ngoja nikapooze koo langu hapo kwa Mama pili.

Wazungu wana utu sana for sure
 
Kuna NGO nilifanya nao first interview last week kwa njia ya zoom meeting,sasa juzi wakanipigia kuwa leo niende kwa second interview pale ofisini kwao mikocheni...
Bora ilo shirika, nimeapply Enabel, sahivi week mbili zimepita,toka deadline lakini kimya Hadi leo
 
Umeona khee Kuna sehemu raha tu unajihisi confidence so huku mnaambiwa kasubirini chini ya tent wengine kweny mawe unapoteza confidence mapema nakumbuka pale kivukoni utumishi.
 
umenikumbusha miaka fulani kuna jamaa nili apply kimchezo mchezo tu ghafla wakanipigia simu tukapiga interview, baada ya siku mbili wakanipigia tena kuwa niende ofisi kwao Zanzibar (arrangement zote walifanya nikakwea pipa......... huyo zenji kufika airport naona Bango la mwenyeji wangu, paap kwenye ndinga hao Ofisini, same day nikafanya interview baada ya interview nakutana na Cashier ananisainisha 60K ya Lunch. baadae nikarudishwa Airport huyo tena nikakwea pipa kurudi Dar!!

Nilipata kazi tulikuwa tunalipwa kibunda hasa..... !!

Asante Mradi wa MKENZA!!
 
Bora ilo shirika, nimeapply Enabel, sahivi week mbili zimepita,toka deadline lakini kimya Hadi leo
Ukishaomba kazi unatakiwa ufanye mambo mengine uwe busy na mambo yako..unashangaa kwenye michakato mara simu hio inaitaa ngrii ngriii wewe ndo fulani ? Karibu kwenye interview au hata email unacheki cheki mara kadhaa...
 
Back
Top Bottom