Nina mashaka na hali ya elimu hapa nchini kwa sababu pamoja na matatizo mengineyo yanayoikabili sekta ya elimu inaonekana walimu wapo katika mgomo baridi. Mashaka hayo ninayapata baada ya kupokea sms zifuatazo kutoka kwa watu nisiowafahamu ambao wanajipambanua kama walimu:
(b) Kipato kidogo ukilinganisha na mwanasiasa?
(c) Alikuwa mvivu?
(d) Aligundua kuwa ualimu ni unyanyasaji na ukandamizaji wa haki?
(e) Alikuwa na madeni mengi mshahara mdogo?
watumaji wa sms hizo wanasisitiza mpokeaji atume sms hizo kwa walimu/watu wengine wasiopungua mia moja
Kama nilivyotangulia kusema nina mashaka na hali ya elimu hapa nchini. Ni nani atakayebadilisha hali hii ya sintofahamu katika sekta ya elimu? naungana na NGO inayoitwa Twaweza wanaposema "NI SISI TWAWEZA"
- Tuungane kuwapongeza walimu wa wilaya ya Kondoa kwa kufelisha shule 47 za wilaya hiyo
- Unajua baba wa Taifa mwenyewe alikuwa hapendi ualimu ndiyo maana aliacha... Wewe unafikiri sababu za yeye kuacha ualimu ni zipi kati ya hizi?