Kuna Mgomo baridi wa walimu?

Kuna Mgomo baridi wa walimu?

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
Nina mashaka na hali ya elimu hapa nchini kwa sababu pamoja na matatizo mengineyo yanayoikabili sekta ya elimu inaonekana walimu wapo katika mgomo baridi. Mashaka hayo ninayapata baada ya kupokea sms zifuatazo kutoka kwa watu nisiowafahamu ambao wanajipambanua kama walimu:

  1. Tuungane kuwapongeza walimu wa wilaya ya Kondoa kwa kufelisha shule 47 za wilaya hiyo
  2. Unajua baba wa Taifa mwenyewe alikuwa hapendi ualimu ndiyo maana aliacha... Wewe unafikiri sababu za yeye kuacha ualimu ni zipi kati ya hizi?
(a) Alikuwa haandai maandalio
(b) Kipato kidogo ukilinganisha na mwanasiasa?
(c) Alikuwa mvivu?
(d) Aligundua kuwa ualimu ni unyanyasaji na ukandamizaji wa haki?
(e) Alikuwa na madeni mengi mshahara mdogo?
watumaji wa sms hizo wanasisitiza mpokeaji atume sms hizo kwa walimu/watu wengine wasiopungua mia moja

Kama nilivyotangulia kusema nina mashaka na hali ya elimu hapa nchini. Ni nani atakayebadilisha hali hii ya sintofahamu katika sekta ya elimu? naungana na NGO inayoitwa Twaweza wanaposema "NI SISI TWAWEZA"
 
Kama vile umeleta post hii kuwachonganisha walimu na serikali vile! Hivi ni mwaka gani matokeo ya level yoyote yametangazwa na hakuna aliyefeli? Kama ni wingi wa kufeli mbona hata miaka michache iliyopita form fours walifeli kuliko hata haya matokeo ya form two wa leo! Anyway ni mtazamo wangu........
 
Mmh sidhani serikali yenyewe inasema watoto wamefaulu sasa haya yako sjui kama yana ukweli

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wewe unajua leo?we shuleni walimu wanachezeshana kibati kwa pesa za tuition A.K.A mkakati chezea matichar wewe
 
Back
Top Bottom