Huyo Pogba mwenyewe nina mashaka na kichwa chake! Jamaa uwezo wake upstairs inaonekana upo chini sana ;mchezaji wa Man Utd mwenye akili zake hawezi kubabaika kwenda Barca au Real ,Manchester ni timu kubwa Duniani same level na huko wachgezaji washamba wengi wanakobabaishwaga! maana Dogo mshahara anaolipwa Old Traford Barca hawawezi kumpa believe me. Sasa timu imempa hela hiyo halafu yeye hataki kuipa respect humo kichwani mwake kuna nini?
Upande mwingine bodi nayo ina nakisi Fulani sababu haiwezekani timu ina uwezo na mapato yanaongezeka kila mwaka halafu mmbanie kocha hela ya kusajili, Wana sababu gani wasimpe hela ya usajili hata kama alipewa hela nyingi huko nyuma?, EPL ya miaka hii ya karibuni hivi kuna kutoboa kweli bila kusajili?