Kuna watu nimewahi kuwasikia kuwa eti kuna miema inakula nyama, je kuna ukweli wowote katika hili?
- Tunachokijua
- Mimea inayokula nyama ni mimea inayopata baadhi au sehemu kubwa ya virutubisho vyake kwa kunasa na kula wanyama au protozoa, mara nyingi wadudu na viumbe wengine wa arthropodi, na wakati mwingine mamalia wadogo na ndege. Mimea hii inapata nguvu zake zote kutoka kwa usanisinuru.
Je, ni kweli kuna mimea inayokula nyama?
JamiiCheck imefatilia na kubaini kuwa ni kweli kuna mimea inayokula nyama na Kuna zaidi ya spishi 583 za mimea inayokula nyama. Mimea hiyo inakula nyama ili kufyonza virutubisho vinavyopatikana kutoka kwa wadudu.
Mifano maarufu ya mimea ilayo nyama ni pamoja na mimea aina ya Venus flytrap (Dionaea muscipula), pitcher plants, na bladderworts (Utricularia spp)
Venus Flytrap (Dionaea muscipula) majani yake yanayofungika haraka ili kunasa wadudu, wanapoingia na kugusa majani hukunjuka na kufunika mdudu, na kisha hufyonza virutubisho baada ya kumeng'enywa.
Pitcher Plants (Nepenthes, Sarracenia, na wengineo) Majani yake yanayofanana na mtungi uliojaa maji yenye enzaimu za kumeng'enya kinachonaswa, Wadudu huvutwa na harufu na wakiingia, wanateleza na kuanguka ndani ambapo hufyonzwa taratibu
Bladderworts (Utricularia spp.) Hii yenyewe hupatikana majini au kwenye maeneo yenye unyevunyevu. Ina mifuko midogo ya hewa inayofanya kazi kama mitego ya kunyonya viumbe vidogo wanapoikaribia.
-Mimea hii huwa inavutia ili kuwanasa wadudu, Majani ya mimea ilayo nyama huwa kama mitego kwa wadudu kupitia harufu na rangi
-Mimea ilayo nyama hutoa kemikali za kumeng’enya (enzaimu) ambazo huvunja au kusaga wadudu kuwa virutubisho vinavyoweza kufyonzwa.
-Mimea ya carnivorous hufyonza virutubisho kutoka kwa wadudu ili kusaidia ukuaji wake katika mazingira yenye uhaba wa virutubisho vya asili.