DOKEZO Responded Kuna mitungi ya kupikia inauzwa kwa wateja ikiwa inapitisha gesi. Hii ni hatari sana

DOKEZO Responded Kuna mitungi ya kupikia inauzwa kwa wateja ikiwa inapitisha gesi. Hii ni hatari sana

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Najihusisha na Uwakala wa nishati ya gesi ya kupikia, ipo hivi... kumekuwa na changamoto ya mitungi mingi inakuja kwetu Mawakala ikiwa na leakage yaani inavujisha gesi na ukiwarudisha kwa Wakala Mkuu anakukatalia.

Anasema akiuchukua anachukua kama mtungi tupu hakuna exchange tena, hivyo Mawakala wanakataa hasara wengine wanawauzia wateja hivyohvyo, hii ni hatari sana kukaa na mtungi leakage nyumbani.

Moja ya sehemu yenye changamoto kama hiyo ni Kigamboni, imenitokea kupitia Kampuni ya Oryx na O Gas mitungi ya 6kg na 15kg huwa na leakage kwenye valve zake.

Pia soma
~
WMA: Wananchi wana haki ya kujiridhisha gesi wanayonunua ina uzito sahihi, wauzaji wawe na mizani
~ Kuna uchakachuaji wa ujazo wa mitungi ya Gesi kwa baadhi ya Kampuni; Wananchi tunaumia
 
Najihusisha na Uwakala wa nishati ya gesi ya kupikia, ipo hivi... kumekuwa na changamoto ya mitungi mingi inakuja kwetu Mawakala ikiwa na leakage yaani inavujisha gesi na ukiwarudisha kwa Wakala Mkuu anakukatalia.

Anasema akiuchukua anachukua kama mtungi tupu hakuna exchange tena, hivyo Mawakala wanakataa hasara wengine wanawauzia wateja hivyohvyo, hii ni hatari sana kukaa na mtungi leakage nyumbani.

Moja ya sehemu yenye changamoto kama hiyo ni Kigamboni, imenitokea kupitia Kampuni ya Oryx na O Gas mitungi ya 6kg na 15kg huwa na leakage kwenye valve zake.
 
Mi nimekaa na mtungi wa 0-gas unaovujisha zaidi ya wiki mbili bila kujua mana harufu ilikuwa inasikika kwa mbali, leakage ilipozidi ikawa inatoa sauti ya kuvuja gas kwenye valve. Nikajaribu kufunga barner mpya bado gas ikawa inavuja. Ikabidi niutoe nje ya nyumba na niurejeshe kwa wakala aliyeniuzia. Nilipomtaka anibadilishie akakataa, mwisho tukakubaliana anipe mtungi mpya kwa nusu gharama.

Kwa kifupi hili tatizo lipo, asante kwa wakala uliyeliripoti.
 
Eeh kweli bana, hii ni hatari sana. Mimi nikitumia gesi huwa najaribu kusikiliza kama kuna hush hush flani karibu na bomba, na pia najaribu kupaka sabuni na maji kuona kama kuna mapovu yanatoka. Sijui kwanini mamlaka hawafanyii kazi hii vizuri, wakati ni bomu la kutegwa.
 
Kuna uwezekano hiyo mitungi ni ile iliyojazwa mtaani
ILE inayotoka kwenye magari ya kampuni husika, sijasikia hilo tatizo

USHAURI; Ukinunua au kubadilisha mtungi, dondoshea maji pale juu kwenye valve; Ukiona dalili yoyote ya maji kucheza kama yanapulizwa ACHA, huo unavuja.

Kudondoshea matone ya maji pale kwenye Valve inaruhusiwa hivyo mtoa huduma asikukataze.
 
Hua kabla sijafunga burner nawasha njiti napitisha ju kwenye valve nione kama Kuna chochote kinatoka
 
Aisee, hii mbona hatari na nusu.

Mawakala wapo kila kona, kila duka kuna mitungi ya gesi.

Ni kheri wafanye utaratibu wawe wachache ila usalama uwepo.
 
Back
Top Bottom