Nimeona body language (lugha ya mwili) ya engineer Hamad Yussuf Masauni waziri wa mambo ya ndani ya nchi na IGP Camillus Mongoso Wambura mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania na Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu ya Polisi ni kama tayari wamepewa mawasiliano kuwa hakuna jinsi lazima muende na maji kwa manufaa ya watawala wabaki madarakani .. cheki clip hii chini ikionesha lugha ya mwili ...
08 September 2024
Kilimanjaro, Tanzania
Kutoka ukumbi wa hoteli ya Weruweru River Lodge Moshi Tanzania
View: https://m.youtube.com/watch?v=A3Ov9FIA7L0Semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Weruweru River Lodge, mkoani Kilimanjaro, Tanzania.
TOKA MAKTABA - 20 Julai, 2022
MAPITO:
KUPANDA CHEO KUWA IGP
Wambura ateuliwa kuwa IGP, Simon N. Sirro apelekwa ubalozi Zimbabwe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 20 Julai, 2022 amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-
• Amempandisha cheo Kamishna wa Polisi CP Camillus Mongoso Wambura, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi.
• Amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.
Wakati huo huo, Mhe. Rais amewateua wafuatao kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jeshi la Polisi: –
• Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Liberati Sabas Materu kuwa Kamishna wa Fedha na Logistiki. Anachukua nafasi ya (CP) Hamad Khamis Hamad.
• Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji.
• Amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Awadhi Juma Haji kuwa Mkurugenzi wa Operesheni Makao Makuu;
• Amempandisha Cheo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Faustine Constantine Shilogile kuwa Kamishna wa Polisi Jamii. Anachukua nafasi ya CP Dr. Mussa Ali Mussa ambaye atapangiwa majukumu mengine.
• Amempandisha Cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamisi Kingai na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)