Kuna Mmasai aliniingiza mjini asubuhi ya jana kwenye mvua

Kuna Mmasai aliniingiza mjini asubuhi ya jana kwenye mvua

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
We Mmasai uliyeniadaa na madawa yako ya mitishamba siku ya jana kwenye mvua, nasemaje, sisi ni Pipo, one day tutameet

Alianza kwa kunitandika dawa ya mvuto wa biashara, akafuatia dawa ya mvuto wa wanawake, akamalizia dawa ya kulifanya pembe la ndovu liwe na hasira kali kwa muda mrefu. "Rafiki Rafiki Rafiki..." Dah!

Asubuhi ya leo nimejidharirisha tu ya bure kwenye mlango wa fremu yangu. Yote tisa, Yaani licha ya kucheka cheka, hakuna hata jimama hata moja lililopita na kunioneshea tabasamu. Imebaki moja tu ya pembe la ndovu, hii sijaitest kutokana na tabia iliyokithiri ya mke wangu kuninyima mizagamuo akisingizia kuwa amechoka. Ni mwezi sasa

We Rafiki uliyekula 20k yangu asubuhi asubuhi siku ya jana, nasemaje, sisi ni pipo. Ili kuniaminisha zaidi, alinibipu ili nisave namba yake, nimletee wateja wengine wengi baada ya mafanikio. Sasa hivi haipatikani

😥😥😥
 
Unatepeliwaje na mmasai? Umeingia lini mjini?
 
Wamasai hakuna dawa hawana ila wanavyojazana hospitali sasa, waoga kishenzi kuumwa.
 
Umetapeliwa na mke anakunyima ww ndo tatizo[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi si Msukuma, mimi Msukumaji 🤣🤣

Aahahahahaaa uko sahihi kabisa, unasukuma wiki....😁😁😁

Hello Push Weekend 😄😄😄😄🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️..
 
Back
Top Bottom