Kuna mpango gani wa Siri wa Uwepo wa Magugu maji katika kivuko cha KIGONGO-BUSISI eneo MWANZA serikali haioni haionj jambo hili?

Kuna mpango gani wa Siri wa Uwepo wa Magugu maji katika kivuko cha KIGONGO-BUSISI eneo MWANZA serikali haioni haionj jambo hili?

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,566
Reaction score
3,234
kuna mpango gani wa Siri wa Uwepo wa Magugu maji katika kivuko cha KIGONGO-BUSISI eneo MWANZA serikali haioni haionj jambo hili??

Magugu maji ni majani yanayoota na kuelea ndani ya maji na yamekuwa yakisukumwa kwa upepo kutoka eneo moja kwenda nyingine.

Chini ni picha ikionesha eneo la ujenzi wa barabara ya juu iliopo kati ya kigongo - busisi - Mwanza lakini maeneo hayo Sasa yamezungukwa na magugu maji kiasi kwamba imesababisha usumbufu wa vyombonvya usafiri majini lakini hakuna juhudi zozote zinazofanyika labda tuulize mnampango gani wa Siri hapo.?

Mambo haya yasingekuwepo wakati wa magufuli maana huo tayari ni uchafu

IMG-20250521-WA0070.jpg
 
Asante ndugu mtoa mada, serikali ya awamu ya sita imeandaa mpango mkakati madhubuti wa kudhibiti magugu yote ziwa Victoria, na kwa kukuhakikishia hilo tumeandaa zana za kutosha tena tutawatumia vijana wazawa ili kupanua wigo wa ajira kwa vijana wetu, Asante.

# Hapo waziri anarekebisha tai anakaa huku mambugira wenzake wanagonga meza kumpongeza kwa jibu zuri FuCkDemAll
 
Ndugu mwananchi, nikiwa kama Waziri wa Uvuvi napenda kukufahamisha Serikali yetu tukufu imetenga kiasi cha Bilion 205 kwaajili ya kuondoka Magugu yote Busisi fery na Kamanga fery. Hivyo msiwe na wasiwasi mpango huu utakamilika mnamo 2093
 
Haya magugu yameanza zamani sana kama mchezo, lakini yameenea hapo ziwani hadi naamini ziwa liwanweza kutoweka baada ya miaka kadhaa.

Juzi Majaliwa alikuwa hapa wanamdanganya na mafyekeo wanafyeka, akiondoka wamemaliza kazi na mabilioni yanaliwa.

Pale tunahitaji vifaa haswa, Majaliwa alisema serikali imesha nunua baadhi ya vifaa na kupeleka wataalamu Uganda kujifunza, na vifaa vingine vinakuja lakini sijui kama watayamaliza, ni mengi yameenea sana.
 
Back
Top Bottom