Kuna mstari mwembamba unaomtofautisha Askofu Gwajima na Kibweteere

Kuna mstari mwembamba unaomtofautisha Askofu Gwajima na Kibweteere

Askofu gwajima namjua vzuri tu, si jamaa wakukurupuka hata siku moja nimchunguzi, anafatilia na details nyingi sana anazo so anachokisema anakijua vzuri ninyi wengne mjibuni kwa hoja au fanyeni kama USA wekeni dola 100 kwa kila atakayechanja
 
Watu wanajifunza kutoka mataifa mengine,watu wana network ambayo mwingine anaweza kua hana,Gwajima si punguani,yamkini anaye mponda hana hata uwezo wa kuwafanya watu sita tu wamsikilize ila yeye ana watu karibu elfu tatu wamfuatao nyuma kuonyesha wazi kuna kitu ndani yake, watanzania tumezoea kusifia na kufuata maneno kama ya kina Malcon X au wengineo wa huko Ulaya na kudharau wa nyumbani mwao.

Zaidi ya yote presha ya Covid-19 ni ya wazungu na wanalazimisha taharuki iwe ya dunia yote, huku Uswahilini kwa 90% hakuna Covidi-19 tusidanganyane na kutishana
Suala la wafuasi anao lakini 90% ni mbumbumbu tu
 
Ni mwarabu kwa shinikizo la wazungu (madalali wa chanjo)
ni waarabu wenyewe hakuna shinikizo hapo. kila nchi i a serikali huru na sheria zake. kwann ushinikizwe wkt una mamlaka kamili ya kukataa?
viongozi wa kiarabu ndio wameamua.. wangetaa isingepita. hakuna cha mzungu hapo
 
ni waarabu wenyewe hakuna shinikizo hapo. kila nchi i a serikali huru na sheria zake. kwann ushinikizwe wkt una mamlaka kamili ya kukataa?
viongozi wa kiarabu ndio wameamua.. wangetaa isingepita. hakuna cha mzungu hapo
Aisee
 
KABLA Joseph Kibweteere, kushawishi mamia ya wafuasi wa kanisa lake kuamini dunia ilikuwa mwishoni, kisha kusababisha vifo vya watu 778, Uganda, dunia ilishakuwa na madhehebu ya Heaven's Gate (Geti la Mbinguni).

Heaven’s Gate ni kanisa lililoasisiwa mwaka 1972 na watu wawili, wa kwanza ni Bonnie Nettles na Marshall Applewhite. Wakahubiri kuwa waumini wao wangefika mbinguni hai, wasingekufa. Kisha, mwaka 1985, Nettles (muasisi wa kanisa), akafariki dunia, kwa maradhi ya kansa.

Kifo cha Nettles, kilitosha kuwa somo kuwa kanisa hilo lilihubiri maono batili. Hata hivyo, wengine wakaendelea kuamini. Mwaka 1996, wanachama hai wa imani hiyo, walikutana kwenye jumba lao waliloliita kwa siri, Air Heaven (ndege ya mbinguni), mjini Rancho Santa Fe, San Diego, California, wakanywa sumu. Wakafa.
Walitarajia Air Heaven ingewapaisha mpaka mbinguni. Walijiua waende peponi ili dunia ipokee mamlaka mpya. Miili yao ilipogundulika mwaka 1997, ilikutwa na ujumbe uliosomeka: “Miaka yetu 22 ya darasani hapa kwenye sayari ya dunia hatimaye inafika mwisho. Tunafurahi kuiacha dunia na kuondoka pamoja.”

Kibweteere, yeye baada ya kukutana na mwanamke kahaba, Credonia Mwerinde, wakatangaza kuokoka. Credonia akajinadi kumpokea Yesu na kuacha kujiuza kimwili. Kibweteere, ambaye alikuwa na shida ya ubongo, kwa pamoja wakaanzisha kanisa waliloliita “Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God” - “Vuguvugu kwa ajili ya Urejeshaji wa Amri Kumi za Mungu.”
Miaka ya 1990, Kibweteere alitoa kitabu alichokipa jina “A Timely Message from Heaven: The End of the Present Time” – “Ujumbe wa Wakati Mwafaka kutoka Mbinguni: Mwisho wa Wakati Uliopo.” Kibweteere na Credonia, wakahubiri dunia imefika mwisho. Waumini wao wakaamini. Wakauza nyumba na mali zao zote, fedha wakampa Kibweteere. Kisha Kibweteere akawateketeza kwa moto. Yeye na Credonia wakakimbia.

KIBWETEERE MPAKA GWAJIMA
Anzia katika mafundisho ya Nettles na Applewhite, kisha Kibweteere, halafu msikilize Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima. Utapata kitu kimoja cha kufanana; ni kuwafanya waumini wao wawaamini na waishi kwa kufuata hisia zao.
Nettles na Applewhite, walijidanganya kuwa wao wangeingia peponi bila kufa. Wakashawishi waumini wao. Nettles akafa kwa kansa mwaka 1985, hakuna aliyeshituka. Applewhite akaendeleza imani. Naye alikufa na waumini wake kwa kunywa sumu.
Gwajima anazo hisia kuwa Waafrika wapo hatarini ama kuteketezwa au kuharibiwa mfumo wao wa kimaumbile na Wazungu, kupitia chanjo za Covid-19. Anatuhumu kuwa wanaotetea chanjo, ni wanufaika wa mgawo wa kifedha kutoka nje. Ametajwa tajiri namba tano duniani, Bill Gates.
Kupitia mahubiri kanisani kwake, Gwajima amewataka waumini wake wakatae chanjo. Akasema, chanjo iliyoletwa nchini ni tofauti na waliyochomwa Waingereza. Akaahidi kuwa yeyote atakayeshinikiza chanjo kutumika nchini bila kuthibitisha ina madhara gani kwa Watanzania, atakufa.
Tutungeneze matawi matatu; la kwanza, kwamba wanaoshawishi Watanzania kuchanjwa ni wanufaika wa fedha. Je, nani anashawishi? Rais Samia Suluhu Hassan, jana alizindua matumizi ya chanjo ya Janssen kwa Watanzania. Janssen, inatengenezwa na taasisi ya kimarekani ya Johnson & Johnson.
Je, anamtuhumu Rais Samia bila ushahidi wowote, kwamba ana malengo ya kuwasababishia madhara Watanzania kwa manufaa ya kifedha? Gwajima ni mbunge kupitia CCM. Rais Samia ndiye Mwenyekiti wa CCM. Je, ni kwa jeuri na kiburi gani, Gwajima anamtuhumu mwenyekiti wake wa chama chake?
Pili, Gwajima sio daktari. Kwa nini anaingilia mambo asiyo na utaalamu nayo? Tatu, kwa nini watumishi wengi wa Mungu wanapenda kutishia watu kifo? Desemba 2016, Kiongozi wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo, alitoa ahadi kwamba waliotoa habari za yeye kuwa mlevi wangekufa kabla ya Machi 2017. Hatujawahi kupata ripoti ya vifo.
Gwajima anapokuja na vitisho vya kifo, ni dhahiri anarejea ya Lusekelo ‘Mzee wa Upako’. Maneno ya vitisho kutoka kwa Yona kwenda kwa watu wa Ninawi, kwamba wangeangamia kama wasingetii neno la Mungu na kuacha maovu, wahubiri wa siku hizi wanayatumia vibaya. Ukimkosea yeye anakuahidi kifo. Ukiruhusu chanjo ya Covid-19 ili kuokoa maisha ya wengi, pia unaahidiwa kifo. Halafu katikati ya hiyo ahadi jina la Mungu linatajwa.
Neno la Mungu katika Biblia linasema “watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", wakati kwenye Kuran, kusoma imewekwa ni wajibu ili mtu mwenyewe aweze kutumia elimu na akili yake kuchanganua mambo. Waumini wanapaswa kujiongeza ili kuchuja yatokayo kwenye vinywa vya viongozi wao wa kiroho na kweli halisi yenye kumwelekea Mungu.
Huu ulimwengu una mabadiliko makubwa. Sayansi hudhibiti uongo. Dunia ya leo si ya mtu kuja mbele yako na kukueleza kuwa Ulaya kila mtu anamiliki Mercedes Benz. Dunia ya sasa ipo wazi mno. Ndio maana, Karne ya 19, mwanafalsafa wa Ujerumani, Karl Marx, alisema: “Maendeleo ya sayansi yanasaidia kuondoa uhalali wa utawala wa wafalme na nguvu za Kanisa.”
Mantiki ya maneno ya Karl Marx ni kuwa ulimwengu wenye maendeleo mazuri kisayansi, hulazimisha demokrasia kutawala badala ya wafalme kuendelea kushika hatamu. Vilevile, viongozi wa dini wenye kutumia porojo kama mtaji, hawawezi kufanikiwa kwenye dunia ya kisayansi.
Mathalan, Gwajima wa leo, hahubiri misukule kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Habari za kumfufua Amina Chifupa, zilishapoteza uhalali na zilifeli. Sayansi ilisaidia Watanzania wengi kutambua kuwa Gwajima aliahidi angemfufua Amina lakini alishindwa. Hata habari ya Gwajima na Edward Sokoine, iliisha kienyeji.
Hata haya maagizo yake kwa waumini wake kwamba wasikubali chanjo, yatapoteza nguvu kisayansi. Watu wakichanjwa na maisha yakiendelea bila matatizo, Covid-19 ikadhibitiwa nchini, mwisho itaonekana Gwajima alikuwa anahubiri yasiyokuwepo duniani wala mbinguni. Kama dhana ya misukule ilivyomshinda, au Amina ambavyo hakukufuka.
Bado kuna yale maono yake ya kugeuza misikiti kuwa Sunday Schools. Akaahidi yeye ni mbeba maono na hatakufa kabla hajatimiza hayo. Mahubiri ya shari kabisa. Siku alipoutamani mlango wa siasa, akajiita Rashid. Udini!
CHANJO YA JANSSEN
Janssen ndio chanjo iliyozinduliwa kwa ajili ya Watanzania kuchanjwa. Wakala wa Dawa Ulaya (EMA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) Marekani, wamethibitisha kuwa Janssen ni salama. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), nalo limeridhia Janssen itumike. Wataalam wa Umoja wa Afrika (AU), wamejiridhisha kwamba ni salama.
Ufanisi wa chanjo ya Janssen ni asilimia 85.4 mpaka 93.1 hadi kwa watu wenye magonjwa sugu na wanaokuwa wamelazwa. Katika kila watu 100,000 wanaochanjwa, hutokea kesi zisizozidi nane za kuzimia. Hiyo ni asilimia 0.008. Hapo ni sawa na hakuna.
Inashauriwa kwa watu wenye matatizo ya mzio (allergy) na sindano za chanjo, wasichanjwe. Kwa ambao hawana shida ya allergy, kwao ni ruhusa kuchanjwa, maana ni salama.
Kuhusu kesi za kuzimia; kwa mujibu wa chapisho la Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa na Kinga (CDC), mtu anapochanjwa Janssen, anatakiwa kupumzika kwa angalau dakika 15, hapo itakuwa rahisi kuepuka kuzimia.



Credit: Luqman Maloto
Kiukweli ukimsikiliza mchungaji gwajima hoja zake,unajiridhisha kwamba kuna watu kawashika kubaya.
 
Marekani waliotengeneza chanjo inawalazimu kutumia pesa kama kivutio ili kuwachanja watu wake.
Wewe uliyepewa bure unataka uwalazimishe watu kuchanjwa? wapi na wapi?
Rais wa marekani ametangaza kuwalipa dola mia moja kila mtu atakayejitokeza kuchanja.
Na wewe kama kuna watu hawataki tumia njia mbadala kuwashawishi.

Hapa kwetu serikali imeleta chanjo na imesema ni hiari mtu kuchanja au kuacha
sasa sisi huku mtaani kwanini tunawashwa na kutaka watu wote wachanjwe?
Gwajima anasisitiza watu watumie hiari yao,na yeye amesema yeye na watu wake hawatachanjwa.
Nakushauri kama wewe ni muumini wa gwajima na unataka kuchanjwa,hamia dhehebu jingine utumie haki yako na hiari yake kuchanjwa.
Siamini kama atakuzuia maana unahaki ya kuchagua mahali pa kuabudia.
 
"Presha ya covid wazungu wanalazimisha kivip and how?
as far as concern hakuna mahali wamandika nchi fulani isipotumia chanjo watakula sanction au kutengwa kimataifa.

ni nchi husika serikali na serikali zao wanaomba wenyewe.. na nchi zingine wananunua kabisa..

Kuna na network kubwa hapa duniani hakukufanyi uwe smart kuliko wengine.. after all ni nothing special coz dunia ni kijiji sikuiz.. mawasiliano yame kuwa kwa kasi so ni rahis watu kupata taarifa..


the only difference hapa unapata taarifa kutoka kwa nani.
Huku duniani kila mtu ana maoni na mtazamo wake kama wewe hapa unaetaka kuamini kua Covid ipo kwa kiwango kikubwa ilihali yamkini hujawahi kuuguliwa au kufiwa na ndugu mwenye Covid,uswahilini kiwango si kidogo tu bali hata hakionekani na maisha ya watu yanaendelea kama kawaida.

So huwezi ponda maoni ya Gwaji kwa sababu ya maoni yako wewe maana hata wewe unachemka vile vile
 
Watu wanajifunza kutoka mataifa mengine,watu wana network ambayo mwingine anaweza kua hana,Gwajima si punguani,yamkini anaye mponda hana hata uwezo wa kuwafanya watu sita tu wamsikilize ila yeye ana watu karibu elfu tatu wamfuatao nyuma kuonyesha wazi kuna kitu ndani yake, watanzania tumezoea kusifia na kufuata maneno kama ya kina Malcon X au wengineo wa huko Ulaya na kudharau wa nyumbani mwao.

Zaidi ya yote presha ya Covid-19 ni ya wazungu na wanalazimisha taharuki iwe ya dunia yote, huku Uswahilini kwa 90% hakuna Covidi-19 tusidanganyane na kutishana
Unamuamini Gwajima?
 
Huku duniani kila mtu ana maoni na mtazamo wake kama wewe hapa unaetaka kuamini kua Covid ipo kwa kiwango kikubwa ilihali yamkini hujawahi kuuguliwa au kufiwa na ndugu mwenye Covid,uswahilini kiwango si kidogo tu bali hata hakionekani na maisha ya watu yanaendelea kama kawaida.

So huwezi ponda maoni ya Gwaji kwa sababu ya maoni yako wewe maana hata wewe unachemka vile vile
sorry umeandika kama unanijua vile kumbe hamna kuti unatunga tunga theory tu. mm niko in science side.. why because it can prove such a viral strain exists?
can gwajima prove what he said scientificaly?

to me gwajima ni politician tu he is not a svientist.

+ siwez weka mambo ya familia yangu publiv places kama hizi. ila nimepoteza ndugu zaidi ya watatu. so najua ninachokisema
 
Back
Top Bottom