digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,508
- 23,368
Yaa serikali imeingilia kati sana kuwaelimisha waachane na hiyo chagulaga system, ilikuwa ni tabu sana enzi miaka ya 90 kurudi nyuma.Daah yaani hapo ndio wamestaarabika. Hali ilikuwa mbaya
kiukweli haya majamaa malugaluga sana.Wasukuma msijifanye hamuelewi
View attachment 3614847
Ukienda huko Katavi unawakuta wasukuma wengi wamevaa hivyoInasikitisha sana kuna sehemu bado nyuma kiasi hiki. BTW hivi wasukuma wanavaa hivi?
Duuh hii ni hatari sanaMpanda mpaka Sumbawanga huku yametawala sana. Imefikia kipindi watendaji wa kata wametunga sheria ya hawa vijana wakionekana katikati ya miji wakifanya hiyo chagulaga ni kukamatwa na kuwekwa ndani maana wamesababisha madhara makubwa kwa raia wanaokutana nao njiani (Wakishangaa wanayofanya kwa watoto wa kike) kwakuwapiga na bakora wanazotembea nazo mpaka kuwapasua vichwa. Nadhani hizo bakora wanazipaka dawa
Waendelee kuwaelimisha wataacha tuYaa serikali imeingilia kati sana kuwaelimisha waachane na hiyo chagulaga system, ilikuwa ni tabu sana enzi miaka ya 90 kurudi nyuma.
Hivyo haya mambo ukienda shinyanga,mwanza ,geita, simiyu ,mikoa ambayo inakaliwa na wasukuma kwa sasa hayupo.
Mimi ni msukuma,lakini nashangaa kuona utamaduni huu kwa Karne hizi, hata mavazi yao tu,mara ya kwanza kuona msukuma anavaa hivyo ilikuwa ni k ni mwaka 2010 nikiwa liwale-lindi baada ya kupangiwa ajira kwa mara ya kwanza,nilishangaa kuambiwa hawa ni wasukuma,Mimi nilijua ni wamasai
Ni kweli kukuta amevaa jezi ya timu ya mpira juu, chini kafunga kanga au sketi nyeusi na mabuti kwa chini, jamaa wana dressing code sio ya karne hii.Wanavaa ndio, pia kuna wakaka wanavaa sketi
Ndio mambo yenu watu weusi hamna ustaarabu halafu mnanyanyasa WanawakeMbona kama unyani fulani hivi!
Ndio, ukienda huko Sengerema, Buchosi, shinyanga na kwingine wapo hiviInasikitisha sana kuna sehemu bado nyuma kiasi hiki. BTW hivi wasukuma wanavaa hivi?
Nafikiri hata Wamasai hawana tena huu Unyani ingawa wanavaa hiviWapo Wasukuma wengi sana vijijini huko wanaovaa hivyo